Manchester United kumpa Ole Gunnar Solskjaer mkataba mpya

Manchester United kumpa Ole Gunnar Solskjaer mkataba mpya

tc_edo

Senior Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
123
Reaction score
98
Baada ya kumaliza msimu (2020 /2021) bila kombe na kupoteza mchezo wa fainali, jumatano 26 mei 2021 dhidi ya Villareal; Manchester United inategemea kumwongezea Koche Ole Gunnar mkataba wa miaka mitatu na kumuunga mkono kusajili wachezaji hadi wanne. Tokea achukue majukumu ya ukocha 2019 Solskjaer amepambana na kufanikiwa katika kukijenga kikosi cha Mashetani wekendu na bado hajakata tamaa.

"Tangu Ole aingie kulikua na project na wachezaji wanaamini katika mfumo huo na huu sio mwisho wa mfumo huo maana kila mfumo una milima na mabonde. Nawaahidi mashabiki hatutokata tamaaa ingawaje tumepoteza fainali." Marcus Rashford akiongea baada ya mchezo wa Fainali.

Upana wa kikosi kwa Manchester United umekua tatizo hasa wachezaji wa pembeni, beki ya kati, mshambuliaji na kiungo hivyo kufanya uhitaji wa usajili wa hadi wachezaji wanne. Nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Manchester United.

Beki wa kati wa Villareal, Pau Torres nae yupo kwenye rada ya Manchester United. Pia tetesi zinaonesha Declan Rice mchezaji wa kati wa West Ham na Ruben Neves wa Wolves ni viungo wanaoweza sajiliwa na United. Erling Haaland ni mshambuliaji ambae United imekua ikimuangalia kwa muda kidogo na kuona akifaa kama straika wako, pia Harry Kane anaondoka Tottenham hivyo yupo sokoni.

IMG_20210527_223804.jpg
 
Si habari njema sana kwetu sisi mashabiki.

Tatizo linakuwa ni nini hasa? Shabiki anaweza kuona na kupanga kikosi kizuri kwa maoni yake ambapo ukiangalia unaona ni kama kingefanya vizuri kuliko kilichochezeshwa, wao wataalamu huwa wanaangalia nini haswa?

Huyu mwenye Project, amesajili wachezaji wangapi yeye kama yeye kwaajili ya kukaa benchi? Ni nani anasajili wachezaji kwaajili ya benchi, tena wa bei mbaya? VDB, Telles, Cavani, James
 
Si habari njema sana kwetu sisi mashabiki...

Tatizo linakuwa ni nini hasa? Shabiki anaweza kuona na kupanga kikosi kizuri kwa maoni yake ambapo ukiangalia unaona ni kama kingefanya vizuri kuliko kilichochezeshwa, wao wataalamu huwa wanaangalia nini haswa?...
Ole anashindwa kufanya maamuzi sahihi kwa muda sahihi. Hilo ndo tatizo kubwa sana kwa huyu jamaa maana anafeli katika vitu muhimu kwa kukosa uamuzi sahihi mfano game ya jana alitakiwa afanye substitutions before extra time ya wachezaji na muda wa before extra time kuisha alitakiwa amtoe De gea maana ana poor record ya penalt since 2016 hajasev penalty.

Cavan kawa promising sana ndo maana kawa regular starter ila so mshambuliaji wa kumtegemea miaka mitatu mbele. Telles mzur ila defending hauko vzur.
 
Cavan kawa promising sana ndo maana kawa regular starter ila so mshambuliaji wa kumtegemea miaka mitatu mbele. Telles mzur ila defending hauko vzur.
Kwanini aliwasajili kwa bei mbaya kama hakukuwa na uhitaji wa lazima wachezaji hao? Maana usajili kama huo tulizoea kuuona kwaajili ya mission maalum, sio benchi!

Aliposajiliwa CR7, tuliona sababu. Vidic pia tulijua sababu, Rio, Valencia, Nani, Kleberson, Chadwick, Tevez, Larson, Evra, Anderson, Forlan, Van Persie, Nistelrooy, Smith, Fortune, etc Wakina Giggs, Keane, Scholes ndo kilikuwa kizazi cha kutengeneza timu, miaka minne wakauwasha moto uliodumu miaka 11, wakipokea na kuwazoesha wageni mfumo wa Utd, leo nani wakufanya hivyo? Mfumo wa Utd ni upi tena siku hizi?

Jezi za City ziliandikwa 93.20 kwenye kola sio? Maana yake ndio ilikuwa mfumo halisi wa Utd ambao umeshapotea, sasa huyu anayedhania kujenga timu, anajenga timu ipi?

OGS ataturudishia kweli ile raha tuliyoipoteza kwa takribani miaka 18 sasa?
 
Apelekwe team B Kubwa haiwezi anatuzingua sana mpuuzi huyu.
 
Kwanini aliwasajili kwa bei mbaya kama hakukuwa na uhitaji wa lazima wachezaji hao? Maana usajili kama huo tulizoea kuuona kwaajili ya mission maalum, sio benchi!..
I don't know brother give him time[emoji355]. Kwa sasa man united mna team nzuri sana msimu ujao mtafanya vizuri ila ushindani ni mkubwa sana EPL komaeni
 
Baada ya kumaliza msimu (2020 /2021) bila kombe na kupoteza mchezo wa fainali, jumatano 26 mei 2021 dhidi ya Villareal; Manchester United inategemea kumwongezea Koche Ole Gunnar mkataba wa miaka mitatu na kumuunga mkono kusajili wachezaji hadi wanne. Tokea achukue majukumu ya ukocha 2019 Solskjaer amepambana na kufanikiwa katika kukijenga kikosi cha Mashetani wekendu na bado hajakata tamaa.

"Tangu Ole aingie kulikua na project na wachezaji wanaamini katika mfumo huo na huu sio mwisho wa mfumo huo maana kila mfumo una milima na mabonde. Nawaahidi mashabiki hatutokata tamaaa ingawaje tumepoteza fainali." Marcus Rashford akiongea baada ya mchezo wa Fainali.

Upana wa kikosi kwa Manchester United umekua tatizo hasa wachezaji wa pembeni, beki ya kati, mshambuliaji na kiungo hivyo kufanya uhitaji wa usajili wa hadi wachezaji wanne. Nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Manchester United.

Beki wa kati wa Villareal, Pau Torres nae yupo kwenye rada ya Manchester United. Pia tetesi zinaonesha Declan Rice mchezaji wa kati wa West Ham na Ruben Neves wa Wolves ni viungo wanaoweza sajiliwa na United. Erling Haaland ni mshambuliaji ambae United imekua ikimuangalia kwa muda kidogo na kuona akifaa kama straika wako, pia Harry Kane anaondoka Tottenham hivyo yupo sokoni.

View attachment 1799785
Wakati mwingine kocha si lazima ufukuzwe unaweza amua kuondoka mwenyewe kama mambo sio mazuri.
Uwa najiuliza ni yupi kocha bora je ni yule anaepata vikombe hata kama timu haipiki pasi nyingi au je ni yule ambae timu yake inapiga pasi nyingi lakini lakini hapati vikombe?
 
Mashabiki wa Manchester United inaonekana moyoni mwao imetokea kumchukia Ole gunnar. ila ukijaribu kuangalia Manchester chini ya Ole gunnar imepiga hatua mbele. Kwanza imeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Embu angalia Liverpool pamoja na kuwa na kocha wao bora lakini ilifikia hatua anagombea kushiriki champions league. Ukiachana na kushika nafasi ya pili, ameifanya Man u ifike fainali ya europa league. Mpeni muda ataifanya Man u iwe timu ya vikombe.
 
Wakati mwingine kocha si lazima ufukuzwe unaweza amua kuondoka mwenyewe kama mambo sio mazuri.
Uwa najiuliza ni yupi kocha bora je ni yule anaepata vikombe hata kama timu haipiki pasi nyingi au je ni yule ambae timu yake inapiga pasi nyingi lakini lakini hapati vikombe?
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Ole hawezi ondoka mwenyewe
 
Back
Top Bottom