Manchester United kutumia mbinu hii kuinasa saini ya Haaland

Manchester United kutumia mbinu hii kuinasa saini ya Haaland

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
1630649312024.png

MANCHESTER United inaamini kwamba itasepa na saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund bila wasi msimu ujao kwa mbinu kali.

United kwa muda mrefu imekuwa ikiripotiwa kwamba inahitaji saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ila mambo yamekuwa magumu.

Kwa sasa wanaamini kuwa ujio wa Cristiano Ronaldo ndani ya timu hiyo akitokea Juventus utawapa nguvu ya kupata saini ya mshambuliaji huyo.

Ikumbukwe kwamba Ronaldo anarejea Manchester United baada ya kupita miaka 12 kwa kuwa alisepa hapo mwaka 2009.
 
Wakala wake mshatutibuana naye, mchezaji wake Pogba hataki kuongeza mkataba. Huyo Halaand mnaweza msimpate akaishia kwenda Madrid au Bayern.
 
Spain hakuna soko la kabumbu tena siyo vilabu tu hata timu ya taifa kushine. Mpira sasa uko UINGEREZA, mchezaji yeyote sasa anataka kucheza ligi ya Uingereza
 
Back
Top Bottom