Manchester United yamtangaza Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wao

DonDonald

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,533
Reaction score
2,709
Timu ya soka ya Manchester United leo imemtangaza Ole GUnnar Solskjaer kuwa kocha wao kwa mkataba wa miaka 3

Solskjaer ambaye December mwaka jana aliteuliwa kuwa kocha wa muda kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wao Jose Mourinho

Solskjaer alikuwa ni mchezaji wao kwa kipindi cha miaka 11, anakumbukwa zaidi kwa kufunga goli la ushindi katika mechi ya fainali ya kombe la Ulaya mwaka 1999 dhidi ya Bayern Munich

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ole Gunnar Solskjaer amekabidhiwa kandarasi ya kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuifunza klabu ya Man United.

Rai huyo wa Norway , 45, aliwasili katika uwanja wa Old Trafford kama kaimu mnmo mwezi Disemba ilikuchukua mahala pake Jose Mourinho.

Solskjaer alihudumu misimu 11 kama mchezaji wa United akifunga goli la ushindi katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya 1999.

BBC
 
Ndani ya miaka 3 hatochukua hata kikombe cha kahawa

Man u wamekulupuka.
 
Baasi!! Manchester wanaanza kwa kutolewa uefa champions league, na matokeo ya kusua sua, wao na Tottenham watagombea nafasi ya 4.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa msimu huu sihesabu chochote kwa kweli. Ole amepewa timu ikiwa na hali tete.
Tulipofikia pia ni mafanikia kiasi fulani japo sio yale washabiki tunataka.

Kutolewa na Barca iliyo na kikosi kipana na form nzuri sio kitu cha ajabu kabisa.(hili wala haliumizi), ila kwenye ligi Top 4 ni kama 3.14 au 22/7πŸ˜›
 
Hakuna maajabu labda bahati. Miaka mingine ya tabu kwa mashabiki wa Man U. Wakikosa Champions League qualification kama hawatamaliza ndani Top Four wachezaji weengi watagoma kusajiliwa. Ni kocha mzuri kwa kuwapa hamasa wachezaji wala hana kiburi illa kwa mbinu bado. Acha tuone killa la heri Ole.
 
Kwa timu ile inayoshinda kwa bahati nasibu,sioni dalili nzuri za huyu Ole, ajipange kisaikolojia tu hasa msimu ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…