Mandhari ya kuvutia angani - Jozi la Sayari mbili jirani na Mwezi hilali

Mandhari ya kuvutia angani - Jozi la Sayari mbili jirani na Mwezi hilali

njiwaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
289
Reaction score
209
Angalia mandhari ya kuvutia sana angani 16 na 17 Desemba, mara baada ya magharibi karibu na upeo wa magharibi: Mwezi hilali jirani kabisa na jozi la Mshtarii na Zohali.

Watch the attractive sight 16 and 17 December of the crescent Moon close to the Jupiter-Saturn pair in the western sky soon after sunset near the west horizon.

Moon MWEZI Jupiter MSHTARII Saturn ZOHALI 16, 17 Dec.png
 
Hivi ndio halisi leo vinavyoonekana angani sasa hivi. Mwezi hilali chini ya jozi ya Mshtarii na Zohali.

The actual view of the sky now with the crescent Moon below the Jupiter-Saturn pair.
6B188EAB-DCCE-4A08-BD54-AAE8B75EE2BE.jpeg
 
Jioni ya Jumapili 20 Desemba Mstarii ilionekana kwa urahisi na Zohali ilikuwa jirani zaidi kama inavyoonekana hapa chini. Picha ya chini yake nimezizungushia boxi ambamo Zohali (Saturn) iko juu na kushoto tu na nukta ya Mshtarii. Picha ya chini yake nimezizungushia boxi ya bluu uweze kuziona kwa urahisi.

Niliweza tu kuziona kama nyota mbili. Tunasubiri kwa hamu kuziangalia kesho (21 Desemba) zikiwa karibu sana kiasi cha kuonekana kama nyota moja jinsi walivyoona miaka 400 iliyopita na ambacho hatutaona hadi baada ya miaka 60 mwaka 2080.

Kesho 21 Desemba, nitakuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania HQ pale Kinondoni kuanzia saa moja jioni kwa hiyo tuungane kusheherekea tukio hili jioni kesho


L1060295=.jpg


Nmezungushia boxi Mstarii na Zohali kukupa urahizi wa kuziona

L1060295=-.jpg
 
Kama tuu nikitumwa dukani kununua dawa ya mbu hua narudi nyumbani kuuliza tena umenituma nini,

hv kweli ntakumbuka kuangalia juu muda huo.?
 
Jioni niliona nikawa najiuliza nyota zinekaaje leo kumbe wataalamu wamesha andika safi fana
 
Jana niliviona hivi vitu nikawa najiambia mwenyewe kuwa moja ni sayari japo siijui sayari gani(inayong'aa sana) na nyingine ni nyota. Asante mtoa mada kwa ufafanuzi zaidi. Leo ntakuwa makini pia kufuatilia
 
Jana niliviona hivi vitu nikawa najiambia mwenyewe kuwa moja ni sayari japo siijui sayari gani(inayong'aa sana) na nyingine ni nyota. Asante mtoa mada kwa ufafanuzi zaidi. Leo ntakuwa makini pia kufuatilia
Leo muda gani? Ni dunia nzima au? Nipo nchi ambayo tunautofauti wa masaa 8 na tz pia naweza ona?
 
Leo muda gani? Ni dunia nzima au? Nipo nchi ambayo tunautofauti wa masaa 8 na tz pia naweza ona?
Jana ilikuwa mida ya saa 12 kuelekea saa 1 hivi. Kuhusu kuonekana dunia nzima pengine mtoa mada atusaidie
 
Back
Top Bottom