Sasa kama hawabadiliki staili ya muziki walioanza nayo ndio hiyo hiyo, sauti zilezile, mashairi yake yake lazima vijana wanaoibuka kwa kujaribu kufuata principal za muziki hata kama hawajasomea watafute waliosoma ili wawasahishishe lazima watapitwa tuu. Hakuna sikio litakalokubali kuendelea kusikia kitu kile kile kila siku. Kuna watu walipata umaarufu sii kwamba wanajua kuimba lakini kutokana na soko wakati huo ama mashairi walioyaimba yaligusa watu bila kuzingatia utaalamu wa muziki wenyewe sasa akitulia tuu bila kwenda kujifunza do -re-mi- fa-so-la- si-do ni lazima huko mbele atakwama tuu