Mandonga apigwe stop kupanda ulingoni

Mandonga apigwe stop kupanda ulingoni

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Nafikiri sasa ni muda muafaka cha chama kinachosimamia mchezo wa ngumi kumzuia Mandonga kupanda ulingoni.

Kwanza huyu jamaa anahatarisha usalama wake, ngumi sio mchezo wa kupanda panda ulingoni kila mwezi.

Pili anaudhalilisha huu mchezo, inaonekana ni kama anafanya comedy.

Tunajua anatafuta ugali wa familia, lakini miiko ya mchezo husika lazima izingatiwe.
 
Kosa lake nini? Kacheza na kusherehesha, karibia michezo yoote duniani ina mbwembwe, mpaka ule wa kujificha una mbwembwe zake.
Huwezi kupigana mapambano matatu ndani ya mwezi mmoja hata kama ni ya kirafiki ngumi sio kama soka au riadha.. jamaa anatafuta umaarufu sana kuna siku itaokotwa maiti ulingoni
 
Nafikiri sasa ni muda muafaka cha chama kinachosimamia mchezo wa ngumi kumzuia Mandonga kupanda ulingoni.

Kwanza huyu jamaa anahatarisha usalama wake, ngumi sio mchezo wa kupanda panda ulingoni kila mwezi.

Pili anaudhalilisha huu mchezo, inaonekana ni kama anafanya comedy.

Tunajua anatafuta ugali wa familia, lakini miiko ya mchezo husika lazima izingatiwe.
Yeye na wote waliowezesha mapambano yaliyofuatia baada ya lile la TKO wametanguliza njaa mbele kuliko miiko sheria na taratibu za mchezo wa ngumi
 
Hata yeye mwenyewe ameshagundua pambano ambalo anapigwa huwa ana-trend zaidi kuliko ambalo anashinda kwaiyo analeta mizaha ulingoni ili apigwe huyu jamaa anatakiwa kupigwa stop atasababisha mchezo wa ngumi uonekane maigizo au comedy fulani hivi
 
Bondia kwa mwaka anatakiwa kupigana mapambano mawili yeye anafanya kama sifa madhara yake hataona sasa hivi ngoja umri usogee kidogo atajuta
 
Nafikiri sasa ni muda muafaka cha chama kinachosimamia mchezo wa ngumi kumzuia Mandonga kupanda ulingoni.

Kwanza huyu jamaa anahatarisha usalama wake, ngumi sio mchezo wa kupanda panda ulingoni kila mwezi.

Pili anaudhalilisha huu mchezo, inaonekana ni kama anafanya comedy.

Tunajua anatafuta ugali wa familia, lakini miiko ya mchezo husika lazima izingatiwe.
Tangu gsm waingilie suala la Mandonga na kupewa jezi ya utopolo hata ushindi wanajaribu kumtafutia kimchongo mchongo.
Utaona waamuzi tayari wamekuwa na utata kwenye kazi zao
 
Huwezi kupigana mapambano matatu ndani ya mwezi mmoja hata kama ni ya kirafiki ngumi sio kama soka au riadha.. jamaa anatafuta umaarufu sana kuna siku itaokotwa maiti ulingoni
mkuu unamjali mandonga au ni wivu tu? Maiti ngapi huwa zinaokotwa watu wakiwa kwenye upambanaji? Hiyo ni ajali kazini. Mwache atumie fursa. Huwa madaktar wanawapima.

Kuna kitu nimekiona mabondia wengi hawampendi mandonga, kwasababu ya mafanikio yake chini ya mwaka mmoja. Wakati wao wamesota miaka nenda rudi. Wamebaki na umaarufu ila pesa hawana.

Hicho chama kinatakiwa kimpongeze kwa kuongeze mashabiki.
 
Sasa usingesema apigwe stop..!! wivu huo..!! Ungesema wasimamizi wa ngumi wasiruhusu michezo zaidi ya mmoja kwa muda fulani..!! Na isiwe kwa Mandonga pekee, but iwe kwa yeyote.

Unapomlenga Mandonga maana yake una jambo kwake
 
kupigwa apigwe yeye kuumia uumie wewe.
Ulishawahi kuingia kwenye ring kupigana?
Mandonga SIO MUOGA WA RING
ring naijua hata anayeshindwa apewe heshima yake
Hakuna ambae amemdharau kwa ajiri ya kupigwa, soma vizuri maelezo
 
mkuu unamjali mandonga au ni wivu tu? Maiti ngapi huwa zinaokotwa watu wakiwa kwenye upambanaji? Hiyo ni ajali kazini. Mwache atumie fursa. Huwa madaktar wanawapima.

Kuna kitu nimekiona mabondia wengi hawampendi mandonga, kwasababu ya mafanikio yake chini ya mwaka mmoja. Wakati wao wamesota miaka nenda rudi. Wamebaki na umaarufu ila pesa hawana.

Hicho chama kinatakiwa kimpongeze kwa kuongeze mashabiki.
Wabongo ndo zenu mnamjaza mtu upepo yakimkuta mabalaa wote mnakimbia, bondia kwa mwaka anatakiwa kupigana mapambano mawili huyu jamaa kwa kwa mwaka huu tu ashapigana sio chini ya mapambano manne
 
Sasa usingesema apigwe stop..!! wivu huo..!! Ungesema wasimamizi wa ngumi wasiruhusu michezo zaidi ya mmoja kwa muda fulani..!! Na isiwe kwa Mandonga pekee, but iwe kwa yeyote.

Unapomlenga Mandonga maana yake una jambo kwake
Nimuonee uwivu kwa lipi mzee baba, mimi sio bondia simjui hanijui.. ninaongelea miiko na taratibu za mchezo husika, kitaratibu na kiafya bondia hatakiwi kupigana zaidi ya mapambano mawili kwa mwaka., bondia gani mwingine anaepanda ulingoni ovyo ovyo tu kama mandonga
 
Ndo ungesema wamkataze kupigana michezo mingi kwa muda mfupi..!! Why wamfungie?
 
Back
Top Bottom