Maneno gani ya dharua uliambiwa yakakuumiza sana

Nakumbuka mwaka 2014 mwanzoni nilienda kufanya interview pale ukonga. Interview ilikua ni ya Jeshi la Zimamoto. Sasa sisi tulikua wengi sana hivyo ili zoezi liende kasi ilibidi wao mainterviewer wajigawe kwenye magroup matatu mule bwaloni.
Ilipofika zamu yangu niliingia na nikaangukia kwenye meza moja yenye wasaili watatu akiwepo mmama mmoja hivi mtu mzima na miwani yake.
Akaniambia nikae. Baada ya kuka akaamza kuniuliza jin langu nani, naishi wapi na shughuli yangu kwa wakati ule ilikua ni nini. Baada ya kumjibu hivyo, ilionekana kama namdanganya (nahisi alinifananisha na mtu mwingine) , na nilipojitetea zaidi akanambia kwa ukali, "shika vyeti vyako uondoke kwanza mdomo wako unanuka"
Kwakweli iliniuma sana hasa ukizingatia nilitokea mwanza kwa ajili ya hiyo interview.

Nilichojifunza baada ya miezi kadhaa ni kutolalamika sana kwani kila kitu kina sababu na Mungu mwenyewe ndie ajuae. Nadhani nilipo hapa ni pazuri zaidi kuliko nafasi niliyokua naitafuta Zimamoto.
 
mkuu pole sana na una moyo,sie wazee wa ngumi mkonon Apo Kama sio teke lazma ningemmwagia matusi
 
Maneno ambayo sitakuja kusahau ni pale nilipo mpiga dogo mmoja hivi mpaka akazimia na hiyo yote sababu ya mazoea ya kijinga ambayo mm huwa siyapendi.

Ndipo mnoko mmoja akaenda kusema kwa mama yake kuwa nimemuua mtoto wake, muda si murefu yule mama akatimba eneo La tukio akionekana kaja kwa Shari
Alivyo fika tu akanitamkia maneno haya nanukuu "wewe Morgan ole wako mtoto wangu awe amekufa kweli utanitambua mm nani lasivyo utamla nyama ww niangalie tu na Sura yako mbaya kama UNAPULIZA MOTO" hii kitu hadi leo inaniumiza sana inanifanya kila nikiona bajaji au piki piki yenye kioo huwa naenda kujiangalia nione hiyo sura ya kupuliza moto inakuaje nawakati huo huwa na act kama napuliza moto huku najitazama.

Ushauri wangu kwa mtanzania yeyote yule asikubali kuitwa 'ana sura kama unapuliza moto'...Maana hili tusi ni zaidi ya fedhea coz nili hakikisha mwenywe na kujionea kuwa kumbe binadamu wakiwa wanapuliza moto ndivyo wanakuwa mbaya vile.

 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kama nauona mtungi wa Bibi yangu kule Moshi,jameni so mliishia wapi
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ mpka naachana na binti yake tulikua hatuongeleshani naye.
 
Pole sana mkuu
 
me ningepigana asee
Nje ya mada kwani huyo ndo ww mkuu kwenye hako kapicha
 
Hahahaha broo vp now yamekuja kama ya mtungi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…