Thomas Brown
JF-Expert Member
- Jan 25, 2025
- 344
- 856
(1) Cherehan - Charan Singh.
Inaarifiwa uyu ndo fundi nguo wa kwanza afrika mashariki na waswahili tukashindwa kutamka jina lake tukawa tuna litamka cherehani.
(2) Kariakoo - Carrier Corps. Ofisi za kikosi cha Jeshi la mkoloni Muingereza cha kubebea vifaa vya kijeshi.
(3) Ndafu - Mzungu alikula nyama safi ya mbuzi kisha akasema "Wonderful" mchagga alishindwa kusema wonderful akaishia kusema tu "Ndafu"
(4) Temeke Wailes - Kulikuwa na Mitambo ya "Wireless" maeneo yale.
(5) Msasani - Kwa Mussa Hassan (Mmakonde akasema "Nchanani)
(6) Frampeni - Frying Pan.
(7) Shokamzoba - Shock absorber.
(8) Kibololoni - Kibo alone. Mlima Kilimanjaro una vilele viwili yaani Kibo na Mawenzi, hivyo ukikaa eneo lile unaona kilele cha Kibo pekee (Kibo Alone) ndio maana mchagga akapaita Kiboboli. Ndugu msomaji, uliwahi kukaa "Kibololoni?"
(9) Dala - Dollar. Zamani dola moja ilikuwa ni sawa na shilingi 5 za Tanzania ndio maana sarafu ya shilingi 5 ilikuwa inaitwa Dala na shilingi 20 ilikuwa inaitwa paundi.
(10) Karakata - Kalkuta. Hili ni eneo la viwanda huko India. Inasemekana Mwalimu Nyerere alikuwa na mpango wa kuiga utaratibu kama wa India wa kulifanya eneo la Karakata kuwa la viwanda kama Kalkuta India.
Ongezea na wewe mkuu wangu....