Maneno maarufu ya Kiswahili yaliyotokana na kukosewa kwa matamashi. Charan Singh - Cherehani

Maneno maarufu ya Kiswahili yaliyotokana na kukosewa kwa matamashi. Charan Singh - Cherehani

(1) Cherehan - Charan Singh.

Inaarifiwa uyu ndo fundi nguo wa kwanza afrika mashariki na waswahili tukashindwa kutamka jina lake tukawa tuna litamka cherehani.

(2) Kariakoo - Carrier Corps. Ofisi za kikosi cha Jeshi la mkoloni Muingereza cha kubebea vifaa vya kijeshi.

(3) Ndafu - Mzungu alikula nyama safi ya mbuzi kisha akasema "Wonderful" mchagga alishindwa kusema wonderful akaishia kusema tu "Ndafu"

(4) Temeke Wailes - Kulikuwa na Mitambo ya "Wireless" maeneo yale.

(5) Msasani - Kwa Mussa Hassan (Mmakonde akasema "Nchanani)

(6) Frampeni - Frying Pan.

(7) Shokamzoba - Shock absorber.

(8) Kibololoni - Kibo alone.

(9) Dala - Dollar. Zamani dola moja ilikuwa ni sawa na shilingi 5 za Tanzania ndio maana sarafu ya shilingi 5 ilikuwa inaitwa Dala na shilingi 20 ilikuwa inaitwa paundi.

(10) Karakata - Kalkuta. Hili ni eneo la viwanda huko India. Inasemekana Mwalimu Nyerere alikuwa na mpango wa kuiga utaratibu kama wa India wa kulifanya eneo la Karakata kuwa la viwanda kama Kalkuta India.

Ongezea na wewe mkuu wangu....
Call me J .. kolomije
Boswadaa. .. Boss wa dar.
 
Kule Saadani kulikuwa na Mwarabu mmoja sitting room kwake aliweka saa ambayo ilikuwa ikipiga alarm(kengele) kila baada ya saa moja na barazani kulikuwa kuna duka,sasa wateja walikuwa wakisikia hiyo kengele wakawa wanamuuliza Mwarabu nini hiyo? Mwarabu anawajibu Saa dani(akimaanisha saa ndani).
Huo ndiyo msingi wa jina la Saadani.
 
Idodomya - Dodoma
Daslamu - Mzizima
Zenji - zanzibar
R-Chuga - ni neno lisilo maana.
 
MWINYI AMANI ni jina la mwenyeji wa kwanza kuishi maeneo ya buguruni ambapo leo hii watu wanapaita BUGURUNI KWA MNYAMANI 📍

TABATA hii ni sehemu ambayo kulikuwa na duka la kwanza kabisa pale maeneo ya matumbi ambapo duka ilo muuzaji alikuwa ni muhindi ni duka pekee ambalo kila bidhaa uliyokuwa unahitaji utaipata kulikuwa kunafulika watu wengi kutoka maeneo mbali mbali, hivyo kwa haraka haraka muhindi alikuwa akiwajibu tu wateja wake wakiuliza kitu fulani kipo? muhindi alikuwa akiwajibu 😁 Ta pata! akimaanisha utapata ndio hadi TABATA 😂 Ta pata
 
(1) Cherehan - Charan Singh.

Inaarifiwa uyu ndo fundi nguo wa kwanza afrika mashariki na waswahili tukashindwa kutamka jina lake tukawa tuna litamka cherehani.

(2) Kariakoo - Carrier Corps. Ofisi za kikosi cha Jeshi la mkoloni Muingereza cha kubebea vifaa vya kijeshi.

(3) Ndafu - Mzungu alikula nyama safi ya mbuzi kisha akasema "Wonderful" mchagga alishindwa kusema wonderful akaishia kusema tu "Ndafu"

(4) Temeke Wailes - Kulikuwa na Mitambo ya "Wireless" maeneo yale.

(5) Msasani - Kwa Mussa Hassan (Mmakonde akasema "Nchanani)

(6) Frampeni - Frying Pan.

(7) Shokamzoba - Shock absorber.

(8) Kibololoni - Kibo alone. Mlima Kilimanjaro una vilele viwili yaani Kibo na Mawenzi, hivyo ukikaa eneo lile unaona kilele cha Kibo pekee (Kibo Alone) ndio maana mchagga akapaita Kiboboli. Ndugu msomaji, uliwahi kukaa "Kibololoni?"

(9) Dala - Dollar. Zamani dola moja ilikuwa ni sawa na shilingi 5 za Tanzania ndio maana sarafu ya shilingi 5 ilikuwa inaitwa Dala na shilingi 20 ilikuwa inaitwa paundi.

(10) Karakata - Kalkuta. Hili ni eneo la viwanda huko India. Inasemekana Mwalimu Nyerere alikuwa na mpango wa kuiga utaratibu kama wa India wa kulifanya eneo la Karakata kuwa la viwanda kama Kalkuta India.

Ongezea na wewe mkuu wangu....
Aisee. Kna mengi sikubaliani nayo japo yanachekesha. Intamkwa Kiboriloni
 
KIPONZERO ni Kijiji kilichopo barabara ya Iringa kwenda Mbeya, Wakati wa ujenzi wa barabara wapimaji walitumia sana neno KEEP ON ZERO kitu kilichofanya wenyeji wafikiri wale wazungu wanasema kiponzero.
Inachekesha lakini sidhani kama ni kweli.
 
Saiti mira - side mirror
Endiketa - indicator
Ribiti - rivet
Hii ribiti nimecheka. Kwa kifupi ukienda hizi local gereji kuna majina ya kuchakua sana. kiwa mji wa Moshi halafu ukute fundi ni m-kibosho ni burudani. Steering wheel = stilingi
 
Back
Top Bottom