Maneno mapya yakiswahili nisiyovutiwa nayo...

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Habari zenu wana kiswahili...

Kwa mara nyengine nimeamua kuibukia huku tena ili nieleze dukuduku langu juu ya maneno kama mawili matatu ambayo sijavutiwa nayo!.
pia ningependa mabaraza ya Kiswahili yayafute na aidha yachukue maoni kutoka kwa wadau kisha ndio wawe wanayarasimisha maneno ambayo yatakuwa yamepigiwa kura zaidi!.

Nafahamu lugha hutohoa maneno kutoka lugha nyengine, hiyo ni sifa na ni kawaida kabisa ya lugha. vilevile lugha huelezea maendeleo ya jamii husika pia, sasa kunakuwa na baadhi ya mabadiriko ya kiteknolojia duniani kwasasa na sehemu ambazo zimekuwa na hayo maendeleo wamekuwa wakija na majina ya vifaa hivyo, kutokana na utandawazi vitu hivyo husambaa sehemu mbalimbali duniani nakufanya mataifa mengine yaliyo na lugha tofauti kutafuta/ kutunga maneno ya majina ya vifaa hivyo kwenye msingi wa lugha zao za asili.

sasa kwa hapa kwetu sijakubaliana na jina hili..
"NDEGE NYUKI". ikiwa na maana ya "drone".
kwanini watumie maneno mawili kuita kitu hicho, na inakuwa kama maelezo!, hivyohivyo binafsi naona inakuwaze kuwa inachanganya ukitegemea neno ndege toka awali limekuwa na maana ya ndege mnyama na ndege kama kifaa kilichotengenezwa na binadamu kwaajili ya kusafiria n.k.

kwa hili la ndege nyuki binafsi naona watunzi kama hawakulitendea haki!, pendekezo watafute jina moja lisilofanana na kitu chengine nakuwa na tafsiri ya maelezo kitu ambacho ni jina!.

Neno jengine ni "AKILI MNEMBA" kwa kiingereza ni "artificial intelligence".
neno akili sina shida nalo, ila mnemba nachofahamu ni kisiwa kipo huko Zanzibar!! sijui tafsiri nyengine ya neno mnemba zaidi ya hiyo!.

turudi kwenye neno lenyewe "akili mnemba" binafsi ningependekeza libadilishwe na liitwe "AKILI SANIFU".
kwa maana hii sanifu ni kitu chakutengeneza, kubuniwa na moja kwa moja hata ukiangalia kwa lugha hii ya wenzetu "artificial intelligence" linajieleza na nafikiri kwa kutumia neno hilo nililopendekeza ni rahisi zaidi ktk jamii yetu, hivyo ningeomba wahusika wajaribu kuangalia neno hili kama wanaweza kulirekebisha ama yatumike yote ili mtu afanye uchaguzi mwenyewe!.

Ni hayo tu karibuni wadau kwa mjadala.
 
Nami nitoe dukuduku langu
Neno lengine sio kiswahili sanifu
Kiswahili sanifu tunasema lingine,kingine ni

Pia Neno Mbashara halifurahishi badala yake iwe matangazo ya moja kwa moja
Maana yake hayarekodiwi kwanza

Kuna Mnyama mwingine wamempa JINA nyegere
Naomba watafute JINA jingine asante
 
uko sahihi...akili mnemba iwe akli sanifu ........limepita......pia napendekeza drone iitwe ....Nishai au bashaha...
 
wewe mkuu umekaa kimatata sana...🤣🤣

kabla hata mambo yako hayajafika kwenye baraza la kiswahili lazima tung'atane meno humuhumu!.
mimi sijakubaliana nawewe neno "matangazo ya moja kwa moja!"
kwasababu limekaa kimaelezo yani sentensi ni kama unatoa maelezo ama tafsiri!, bora waache hiyohiyo mubashara!.

haya "Nyegere" anashida gani nawewe..?
kwasababu huyu mnyama ni moja ya mnyama mbishi na anapenda sana kulinda jike wake yani anawivu kupindukia!, hata nzi akitua kwenye uchi wa jike lake basi anaweza kumlalua huyo nzi vibaya mno!, kwa sifa hiyo jina nyegere naona linampendeza sana!.
sifa nyengine aliyonayo ni anakinyampo kikali sana akienda kunyampa kwenye mzinga wa nyuki basi nyuki wote wanakimbiana na yeye anakula asali na ndio maana kwa kiingereza akaitwa "honey badger".
 
nishai na bashasha mbona tayari yana tafsiri zake!
 
1. "Kinyampo" ni neno la kilugha au ni la kiswahili sahihi mkuu? Mm najua ni Kijambo au Kujamba i.e. kutokwa na hewa iliyotumboni kupitia njia ya haja kubwa. Halafu kijambo hakiwezi kuwa kikali ila kinaweza kuwa ni chenye harufu mbaya (Foul smell) au harufu kali (Offensive smell au pungent smell).
2. Kulikuwa na neno au msemo uliotafsiri maneno au sentensi ya "Feed back". Mimi nilishindwa kulitumia neno "Mshindo nyuma" ila natumia neno "Mrejesho".
Wataalam hebu niwekeni sawa hapo. Hilo la kwanza la "mshindo nyuma" limekaa kihuni flan hiv. Asante.
 
achana na kijambo na kinyampo sijui neno sahihi ila hili la mshindo hivi hawa wazee wa kiswahili wanatuonaje...?🤣🤣
 
Kisimbuzi kibadilishwe jina kiitwe Kiwiu, asante...
muwe mnasema na kwanini, kisimbuzi ni kitu kinachosimbua.. kusimbua ni kutafsiri mawimbi hiyo ndio kazi ya kisimbusi so mimi naona ni sahihi labda kwenye hili unachuki zako tu..🤣
 
Nami nitoe dukuduku langu
Neno lengine sio kiswahili sanifu
Kiswahili sanifu tunasema lingine,kingine ni

Pia Neno Mbashara halifurahishi badala yake iwe matangazo ya moja kwa moja
Maana yake hayarekodiwi kwanza

Kuna Mnyama mwingine wamempa JINA nyegere
Naomba watafute JINA jingine asante
Jingine Si Kiswahili Sanifu Bali Ni Lingine
 
Back
Top Bottom