KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Habari zenu wana kiswahili...
Kwa mara nyengine nimeamua kuibukia huku tena ili nieleze dukuduku langu juu ya maneno kama mawili matatu ambayo sijavutiwa nayo!.
pia ningependa mabaraza ya Kiswahili yayafute na aidha yachukue maoni kutoka kwa wadau kisha ndio wawe wanayarasimisha maneno ambayo yatakuwa yamepigiwa kura zaidi!.
Nafahamu lugha hutohoa maneno kutoka lugha nyengine, hiyo ni sifa na ni kawaida kabisa ya lugha. vilevile lugha huelezea maendeleo ya jamii husika pia, sasa kunakuwa na baadhi ya mabadiriko ya kiteknolojia duniani kwasasa na sehemu ambazo zimekuwa na hayo maendeleo wamekuwa wakija na majina ya vifaa hivyo, kutokana na utandawazi vitu hivyo husambaa sehemu mbalimbali duniani nakufanya mataifa mengine yaliyo na lugha tofauti kutafuta/ kutunga maneno ya majina ya vifaa hivyo kwenye msingi wa lugha zao za asili.
sasa kwa hapa kwetu sijakubaliana na jina hili..
"NDEGE NYUKI". ikiwa na maana ya "drone".
kwanini watumie maneno mawili kuita kitu hicho, na inakuwa kama maelezo!, hivyohivyo binafsi naona inakuwaze kuwa inachanganya ukitegemea neno ndege toka awali limekuwa na maana ya ndege mnyama na ndege kama kifaa kilichotengenezwa na binadamu kwaajili ya kusafiria n.k.
kwa hili la ndege nyuki binafsi naona watunzi kama hawakulitendea haki!, pendekezo watafute jina moja lisilofanana na kitu chengine nakuwa na tafsiri ya maelezo kitu ambacho ni jina!.
Neno jengine ni "AKILI MNEMBA" kwa kiingereza ni "artificial intelligence".
neno akili sina shida nalo, ila mnemba nachofahamu ni kisiwa kipo huko Zanzibar!! sijui tafsiri nyengine ya neno mnemba zaidi ya hiyo!.
turudi kwenye neno lenyewe "akili mnemba" binafsi ningependekeza libadilishwe na liitwe "AKILI SANIFU".
kwa maana hii sanifu ni kitu chakutengeneza, kubuniwa na moja kwa moja hata ukiangalia kwa lugha hii ya wenzetu "artificial intelligence" linajieleza na nafikiri kwa kutumia neno hilo nililopendekeza ni rahisi zaidi ktk jamii yetu, hivyo ningeomba wahusika wajaribu kuangalia neno hili kama wanaweza kulirekebisha ama yatumike yote ili mtu afanye uchaguzi mwenyewe!.
Ni hayo tu karibuni wadau kwa mjadala.