Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,518
- 6,506
Lugha ngumu nyie
Zote ni kitu kimoja. Zinatofautiana viwango tu.
Uasherati ipo juu.
Zinaa- inatokana na neno Zini. Zinaa ni 'nomino' na Zini ni 'kitenzi'
Uasherati- Ni kwa mtu ambae hajaoa au kuolewa kufanya ngono.
Uzinzi- mtu kutoka nje ya ndoa yake.
(mawazo yangu tu)
zote dhambi.....:shetani:
Asanteni kwa ufafanuzi, ila nilivyowaelewa(sijui kama kichwa changu kigumu) ni kwamba kwa ujumla maneno hayo matatu tafauti, katika matumizi yake hakuna tofauti.
Zinaa- inatokana na neno Zini. Zinaa ni 'nomino' na Zini ni 'kitenzi'
Uasherati- Ni kwa mtu ambae hajaoa au kuolewa kufanya ngono.
Uzinzi- mtu kutoka nje ya ndoa yake.
(mawazo yangu tu)
uko sahihi ila niongeze kidogo kuwa uzinzi ni tabia ya kufanya zinaa. kimsingi hata uasherati ni aina mojawapo ya uzinzi. so uzinzi unacover vyote. hata mtu amabye hajaoa akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke wake na hivyo ni uzinzi pia. na huu ndio uliopewa jina uasherati ila bado kimsingi ni uzinzi uleule. kuna mtu ametaka kujua na ngono pia ni nini? ngono ni tendo la kijamiiana ama coitus kwa kingereza. ni neno laini kutamka kwa kiswahili kwa mujibu wa maadili yetu ila kuna neno gumu kidogo kutamka ama kuandikika na naamini unalielewa. mara nyingi tabia ya uzinzi hujuimuisha ama hukamilishwa na kukolezwa na zawadi ya tendo ngono, ila in some circumstances waweza kuwfanya uzinzi bila ngono kufanyika. kibiblia, tendo lolote la kunajisi imani pia hufananishwa na uzinzi, mfano kuabudu sanamu nk
.............. hata mtu amabye hajaoa akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ni kusema kuwa anafanya mapenzi na mtu asiye mke wake na hivyo ni uzinzi pia. ................
Nenda kaangalie mwenyewe,nimetafuta jinsi ya kukutwangia thanks mbili imeshindikana ila ulikuwa unastahili.
Kama nimekuelewa vizuri ni kama haukubaliani na mnyumbulisho alioutoa Babkey hasa baada ya kuonesha kuwa zinaa ndo shina huku uzinzi ikiwa ni tabia ya kufanya zinaa,je hakuna maneno yanayotofautisha kati ya zinaa ya aliye katika ndoa na ya yule ambaye hayuko katika ndoa.Kwani mfano ulioutoa wa uasherati haukusema kama mwanamke nae hajaolewa au yuko ndani ya ndoa.Utanisamehe wengine ni slow learners.