WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Leo nilikuwa kwenye ibada, ikawepo haja ya kutafsiri neno "Ghost" basi mhubiri akasema "Mzuka"... mbona miguno na vicheko vilitawala!
Nikawa najiuliza mhubiri hajui kuwa "Mzuka" ina maana tofauti kabisa?
Nikazidi kujiuliza, kuna maneno mengi tu siku hizi ukiyatamka watu hupata maana tofauti.
Mfano mzuri ni tangazo la radio kuhusu utumiaji wa pombe.."ulevi noma!".... hili tangazo kuna siku lilizusha mjadala mkali sana.Vijana walikwa wanashangaa iweje tangazo la polisi kusifia pombe?...
Wajuzi hebu tuangalie baadhi ya maneno yenye maana zaidi ya moja tena maana zenye kukinzana.
1. Mzuka -inamaanisha mtu aliyekufa lakini pia lina maana nyingine kabisa ....
2. Noma - hebu tufafanulieni maana yake...
Ongezeeni na mengine.
Inawezekana kabisa kukawa na thread yenye kuzungumzia jambo hili.Kama ipo basi naomba mods muunganishe lakini tuendelee kupeana shule ya kiswahili.
Asanteni