Maneno ya Dkt. Bashiru ni shambulizi kwa Rais Samia na yenye ajenda ya siri. Aitwe haraka na kuhojiwa na chama

Tanzania inaangamia kutokana na UPUMBAVU kama hawa.
Tangu huyo mtu wenu aingie madarakani Nchi hii imekuwa na Mambo ya Ovyo kabisa kuwahi kutokea.
1. Yeye ni kiguu na njia kwenda kuomba mikopo. Akifika nayo tu, MAJIZI yanadaka juu kwa juu, hivyo hiyo mikopo inawasaidia wachache.

2. Tangu aingie madarakani kumekuwa na:-
I. Uhaba wa umeme.
II. Uhaba wa maji.
III. Kupanda kwa bei za vitu.
IV. Ujambazi na mauaji ( Panyaroads)
V. Upigaji wa fedha za umma.

Hayo yote yanatokea lakini hatujawahi kusikia akichukua hatua Mujarabu ili kuinusuru Nchi.
 

Lipost lirefu wakati huwa mnahadaa watu kuwa CCM kuna demokrasia!
 
Bashiru kawashika kusikodhaniwa.
 
Nchi yetu siyo kisiwa na hatuwezi kujifungia ndani tu bila kushirikiana na wenzetu. Safari za mh Rais zimekuwa na faida na mafanikio makubwa Sana kwa Taifa letu, Ni safari na ziara hizi zimesaidia kuvutia wawekezaji na mamillion ya watalii hapa nchini, Ni safari hizo ambazo tumeshuhudia wawekezaji na watalii wakimiminika hapa nchini hasa baada ya wazo la kibunifu la mh Rais la royal Tour lililosaidia kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii pamoja na fursa mbalimbali za kiuwekezaji zinazopatikana nchini mwetu.Ni uwekezaji Huu ambao umezalisha fursa mbalimbali za ajira kwa vijana na kuongeza makusanyo ya mapato, Ni Ziara hizi ambazo zimefanya China kutusamehe Deni la Billion 31 pesa ambayo tutaitumia kuwekeza katika huduma zingine au miradi mingine itakayo wasaidia na kuwagusa watanzania, Ni safari hizo ambazo leo hii mazao yetu yanaingia nchini kenya bila shida na hivyo kufanya soko kuwa la uhakika kwa wakulima
 
Hivi hii nchi vijana wetu wamebaki kuwa machawa tu.Hatuwezi kumukosoa Rais ili afanye marekebisho kwenye utendaji wake?Akili zetu ni kusifia tu na kuweka namba za simu ili tupate uteuzi.Nyie machawa ,ili mjue kuwa ni wapumbavu Kama alivyosema Mkapa marehemu ,nendeni kwenye comments za You tube zote zilizokopi mipasho yenu .Kuanzia chawa Msukuma,Chawa wa UVCCM,Chawa Kigwangara na wengine wote.Comments za watu zinawaponda sana machawa na kumtetea Kakurwa Dr.Kwa hiyo huu ujinga wa kusifia kila kitu ,wananchi hawakubaliani nao.Ni ukosefu wa akili kabisa.Mm binafsi namkubali Rais wetu Kama ,Rais anayejitahid lakin akikosea siwezi kumsifia.Na Kama ningekuwa na bahati ya kukutana nae ,ningemweleza ukweli kuwa Makamba,Nape,Ridhiwani hawafai kuwa mawaziri ni mizigo tupu.Kwa Sasa hatuna maji ,umeme tunasifia nn?Tunaweka namba za simu za uchawa ili iweje?
 
Hongera kwa kuweka na namba ya simu..ila pole ccm inawenyewe awamu hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jibu hoja mkuu

Hoja gani upuuzi mtupu. Rais ndio anatakiwa aitwe ahojiwe kwanini umeme umemshinda, na maji hakuna. Mnaona jambo la maana kumtetea rais aliyefaulu baada ya kutetea nchi kwenye mambo ya msingi.
 
Raisi hajawahi kukosea au yeye hakosei? Kwamba yeye ni mkamilifu muda wote?

Ni upumbavu na ujinga wa hali ya juu kusifia kila kitu.

Unataka kila mtu awe na mawazo kama yako ya kusifia viongozi hata wakifanya vibaya?

Kwa Akili kama hizi ni bora mkoloni arudi kutawala Afrika..!
 
Jamani nadhani namba ya simu mmeiona , huyu kijana anunuliwe simu mpya ili aendelee kumfagilia mama , Simu yake kioo kina Ukungu , mimi natuma elfu 50 sasa hivi
Hata Bashiru kabla ya kumpata yaliyompata, alikuwa msifu wa JPM, leo akili zmemrejea sasa anatema chechee!! Hata huyu Kijana wa Mbozi Igamba, akili zikimkaa vizuri atageuza mapambio,Njaaa mbaya Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…