Maneno ya Dkt. Bashiru ni shambulizi kwa Rais Samia na yenye ajenda ya siri. Aitwe haraka na kuhojiwa na chama

Kwa mawazo yangu, kila nafasi inaenda na wajibu mahususi!! Mtu akikubali nafasi fulani ina maana anakubaliana na wajibu unaohusika kwenye nafasi hiyo!!! Mtu anapotekeleza wajibu wake kwa mujibu wa nafasi yake hawezi kudai sifa kinyume chake inabidi ashukuru kwa kupatiwa hiyo fursa ya kuwatumikia wananchi maana angeweza kupatiwa mwingine na akatekeleza wajibu wake huo huenda vizuri zaidi. Kwa mantiki hiyo mtu yeyote hana haki ya kudai sifa anapokuwa anatekeleza wajibu wake, kiasi cha kutishia wale ambao hawaoni ulazima wa kumsifu kwa kutekeleza wajibu na majukumu yake!

Japo siyo dhambi kama mtu akaamua kumsifu mtu kama njia ya kumtia moyo kwa kutekeleza majukumu yake vizuri, ila asidai na asinune kama ikatokea hajasifiwa!! Isiwe issue kwamba amesifiwa au hajasifiwa!! Ila ni issue kama hajatekeleza wajibu wake! Kila mwenye nafasi katika jamii ana wajibu wa kimaadili wa kutekeleza majukumu yake bila kudai chochote mbali na mshahara au posho yake!! Wakati wa kuomba kura huwa ni wanyenyekevu sana na huahidi kuwatumikia kwa moyo wote wananchi, itakuwa ni ajabu tukafika mahali tukaanza kudaiana sifa kwa nguvu na vitisho eti "aitwe ahojiwe" ebo!!!! MWASHAMBWA SOMA HIYO!!!

Wajibu wa mheshimiwa ni kutekeleza ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHETU!! Anapofanya hivyo anaonesha uaminifu kwa wananchi kwa kutekeleza yale aliyoahidi kwenye kampeni ya uchaguzi!!!
 
Mh Rais ametekeleza vyema kabisa Yale yaliyo katika ilani ya chama chetu na anaendelea na utekelezaji wake kwa kadri ya uwezo wake ndio sababu ya kumiminiwa sifa na pongezi kutoka kwa Wananchi wanaotumikiwa na mh Rais. Sasa kwanini wananchi Hawa wanaoona kwa macho yao kazi njema iliyofanywa na mh Rais na kutoa pongezi na sifa kwa hiyari yao wazuiwe kufanya hivyo? Kwanini wakatishwe Tamaa? Kwanini waambiwe wasimpongeze kiongozi wao? Huoni huko ni kutaka kumkatisha Tamaa Mh Rais?
 
Hayo aliyotoa Bashiru ni mawazo yake binafsi! Hata kama si mawazo mazuri kwa mtazamo wako lakini bado hajavunja sheria yoyote kutoa mawazo hayo kama raia wa Tanzania. Hajamtishia mtu kuwa atamwita kumhoji kama akimsifu mheshimiwa!!! Mpaka hapo yuko sahihi kwa mujibu wa mawazo yake hayo ambayo hullazimiki kuyakubali!! Tatizo lako ni kwamba wewe unalazimisha awe na mawazo kama ya kwako kiasi cha kumchongea aitwe na ahojiwe! Tukianza kuhojiana kwa kutoa mawazo hapo tutakuwa tumeingia kwenye utawala wa KIDIKTETA!!! Silazimiki kumsifu mtu anayetimiza wajibu wake vizuri ila nalazimika kumhoji mtu asiyetimiza wajibu wake vizuri!!
 
Kumwita Bashiru na kumshambulia ni kinyume na katiba, kwani anahaki ya kuongea mawazo yake bila kutishwa. Mawazo hayo ni yake na wengi wameonyesha kuzungumzia humu jamvini. Nchi imekuwa ya kutukuza viongozi badala ya kuangalia maendeleo na direction tunayoendea, mwananchi anaelipa kodi yake imegeuka ni ya Rias wa Jamhuri na kutumia kodi hii ya wananchi imegeuka hisani ya Rais na ni yeye kutoa huu ni upotoshaji wa hali ya juu. Turudi kwenye mstari, na kusema serikali imefanya hiki na kile, kwa kufuata jinsi wawakilishi wetu walivyoipitisha na sii hisani ya viongozi wala CCM. Nakumbuka kumsikia waziri akisema serikali ya ccm imejenga barabara KM kadhaa je CHADEMA wajenga KM ngapi huu ni wenda wazimu, kodi ilipwe serikali ya CCM na barabara ijengwe na CHADEMA huu ni ufutuhi.
 
Niambie mh Membe,mh Kinana na mh Makamba waliitwa Na mh Dr Bashiru wakati ule kwa kosa lipi? Je hawakuwa wametoa maoni yao tu?
 
Niambie mh Membe,mh Kinana na mh Makamba waliitwa Na mh Dr Bashiru wakati ule kwa kosa lipi? Je hawakuwa wametoa maoni yao tu?
Hatujasema kuwa alipowaita alikuwa sahihi!! Naomba kusisitiza kuwa tuongee hoja za msingi na tujadili hoja na si watu!! Hoja ya msingi ni kuwa raia wa Tanzania anayo haki ya kikatiba ya kutoa mawazo yake binafsi ili mradi havunji sheria!!! Mtu yeyote yule akienda kinyume na hilo anafanya kosa bila kujali ni wewe au ni mimi au yeyote!!
 
Mna hari mbaya sana na ndo wananchi washamalizana na nyie na ishakula kwenu hivyo. Kama mtu mmoja kawapasua hivi hao wengine wakija mnapona kweli? hivi nani kawaambia Bashiru ni Bashiru pekee?

Kwa ninavyowaona mmeshachelewa gari na hamkujiandaa kwa lolote, mlilewa mvinyo n haya yamekuja kama surprise kwenu na sasa ni muda wa kupigwa. Poleni kwa kufumwa
 
Dr BASHIRU ametoa maoni kwa mujibu wa katiba ya JMT hajatukana mtu sijaona kosa lake

Hv neno kustaafu au mstaafu lina maana gan


BASHIRU hajawah kustaafu U KM wa CCM Wala u KATIBU MKUU KIONGOZI

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Bila shaka umeachwa njia panda, hujui ushike lipi uache lipi. Hiyo ndiyo shida ya wanafiki. Huku wataka na kule wataka, yote umekosa. Angalia tu usije ukapasuka msamba.
Nimekwepa kabisa kuingia mtego wa kuwa mfuasi wa mtu kwani huwa anapita kama mchanga wa ufukweni na kubakia historia ndani ya muda mfupi sana.

Uchambuzi wa sera ndio mpango mzima. uchambuzi wa masuala yanayogusa maisha ya mtu mmoja mmoja ndio akili zaidi kuliko kusimama nyuma ya picha ya mwanasiasa leo yupo kesho hayupo.
 
Majawabu ya umeme na maji ndio huu migao?
Tindo ondoa wasiwasi mkuu kuhusu Hilo maana umeona mikakatii ya serikali yetu Katika kukabiliana na changamoto hizo, katika maji umeona mh Rais akizindua mitambo mikubwa ya kuchimba visima virefu vitakavyosaidia kupunguza uhaba wa maji ,hata katika umeme nako Ni hivyo hivyo mikakati inafanyika
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuitikisa CCM,hayupo mtu huyo na bado hajazaliwa bado,Kama huamini ondoka CCM au mwambie yeyote atoke ndani ya CCM na umuunge mkono uone Kama ataweza kuitikisa CCM au kuyumbisha. Ukitoka CCM hata wananchi wanakuwa hawana habari na wewe maana Wana Imani na CCM yao na kuiunga mkono
 

Na wale waliopiga makofi unawasemaje? Nao waitwe?
 
Na mie huyo mtu bado simuoni kwa leo Ila hilo lisitudanganye kwamba chama chetu kitakaa milele yote.

Kinachotokea leo kinachokwenda kutokea ni kwamba chama kinatakiwa kujisahihisha kwa kurudi kwenye misingi yake, mabwanyenye hawana nafasi ndani ya chama na hili tunatakiwa kupambana nalo mimi na wewe kwa kuungana. Tukifanya hivi hakika chama chetu kitakuwepo miaka mingi ijayo

Mabwanyenye out
 
Dr BASHIRU ametoa maoni kwa mujibu wa katiba ya JMT hajatukana mtu sijaona kosa lake

Hv neno kustaafu au mstaafu lina maana gan


BASHIRU hajawah kustaafu U KM wa CCM Wala u KATIBU MKUU KIONGOZI

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ukishakuondolewa katika nafasi yako na kuteuliwa mtu mwingine Kama ilivyokuwa kwa Dr Bashiru Basi unahesabika Kama mstaafu
 
Kila wakati najiuliza swali hili kwa nini katika siasa akili kubwa hutumia mbinu ya mirusi mingi. CCM wamekurupushwa kutoka usingizini wanahaha kuwinda mirusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…