Maneno ya kocha Eric Ten Hag baada ya tuhuma za Ronaldo

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
"Tulimpa chaguo la kuondoka msimu wa joto lakini hakupata timu. Tulijaribu chelsea wakakataa, Ac milan wakakataa. Tukamwambia atafute timu lakini hakupata, anazungumzia heshima gani?"

"United imekuwa na wachezaji wazuri siku za nyuma lakini hawajawahi kuwakatisha tamaa hivi. Ronaldo lazima atulie na aelewe kuwa hata simba huzeeka."

My take:
Huyu kocha anaoneka mstaarabu sana, mara zote akiulizwa kuhusu ronaldo amekuwa akisema hauzwi na yupo kwenye mipango yake kumbe anajua kinachoendelea.

Hii imempa thamani ronaldo, iwapo angesema anauzwa na timu akakosa ingekuwa fedheha kubwa sana kwake.

huyu ronaldo kama anajiona mjanja asepe pale kama atapata timu, vigogo wa timu zote kubwa ulaya walimkataa halafu bado analeta kiburi.

Jamaa inaonekana ana kiburi na dharau sana huyu. Asepe zake hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.
 
Mi ni moja ya mshabiki wa Ronaldo lakini nilichogundua huyu jamaa ni mzungu mwenye uswahili mwingi

Naamini hata kwenye kundi la wanaomkubali Messi over Ronaldo, wapo watu wa Ronsldo walioenda kwa Messi kutokana na nidhamu mbovu ya Ronaldo

Matukio mengi ya ajabu mpaka kuna muda nashindwa kumtofautisha na Morrison
 
Mashabiki wa Ronaldo tulikua tunawaambia kila siku lakini hamsikii. Pendu hana jipya analolifanya uwanjani kama asipofunga. Sasa umri umemkamata, anatafuta watu wa kutoa kafara!

Kale ka Andunje sasa hivi kamerudi kati, kanapiga assist za aftatu kila mechi. Kakitenga faul kipa anatetemeka. Akina Mbappe wanakimbia tu hovyo then wanashangaa Andunje amepiga pass imefika. Hii ndio maana halisi ya mchezaji bora!

Sasa kinachomuuma huyu bishoo wenu, ni kwamba Andunje yuko kweny club nzuri yenye potential ya kushinda UEFA, na bado huko team yake ya taifa ni moja ya favourites kwenye kushinda kombe la dunia. Hapo ndipo panapompa degedege bwana Pendu.


Wakati ni ukuta. Ronaldo akubali tu, you can't stay fresh forever. Amefanya mengi makubwa na kuweka rekodi nyingi za kutisha. Ajiandae kisaikolojia, amalize kwa heshima. Hii ego yake haitamsaidia chochote. Ndio maana clubs zote kubwa zinamkataa sasa hivi.

It's time to say goodbye Ronaldo!
 
Ronaldo akiwa Madrid alisema atastaafu soka akiwa na miaka 40, hivyo makocha wamvumilie asije akapata msongo wa mawazo!

Yote kwa yote Ronaldo hataki kukubali kwamba, muda wake umepita!

Aende hata timu ndogo za Ulaya kama bado anataka kuendelea kusakata kabumbu la ushindani!
 
atakufa kwa stress kila jambo lina watakati wake.. Ronaldo ameshamaliza msimu wake astaafu tu.
 
😅😅 Morrison wa ulaya
 
Huyo kocha career yake nzima anakombe gani la maana kumzidi Ronaldo, hayo maneno wangesema kina Pep, Klopp, Carlo , Mou nk ila sio huyo kocha wa timu ndogo
Hata kama ana makombe yanayojaza dunia nzima hakuna mcheza aliyemkuu zaidi ya kocha au timu..

Kumbuka hayo makombe hakuyabeba akiwa peke yake uwanjani, ndiyo maana ikaitwa timu..

"Ameyakwaa sasa anaaibika,kumbe hadi ac milan walimkataa!...what a shame!...
 
Huyo kocha career yake nzima anakombe gani la maana kumzidi Ronaldo, hayo maneno wangesema kina Pep, Klopp, Carlo , Mou nk ila sio huyo kocha wa timu ndogo

Makombe kabeba ronaldo au timu alizochezea ndio zimechukua kwa uwezo wao? Si alikuwepo chini ya sosha kuna kombe kabeba kama ronaldo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…