Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha

Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha

Really?Sio kweli,watu wa hivi huishi muda mfupi sana kwa kuwa wanazama kwenye dhambi,na kumbuka kwamba dhambi inaua,na Mungu sio mwanadamu hata adanganye.

Warumi 6:23 inasema,
"23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."

Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha.

“Nimefikia kilele cha mafanikio katika ulimwengu wa biashara. Katika macho ya wajinga, maisha yangu ni mafanikio. Hata hivyo, kando na kazi yangu, nilikuwa na furaha kidogo sana.Mwishowe, utajiri ni ukweli tu ambao nimeuzoea.

Katika wakati huu, nikiwa nimelala katika kitanda changu cha hospitali, na kukumbuka maisha yangu yote, ninatambua kwamba umaarufu wote, na utajiri ambao nilijivunia sana, umebadilika na kuwa duni mbele ya kifo kilichoko mbele yangu..

Unaweza kuajiri mtu aendeshe gari lako au kupata pesa kwa ajili yako, lakini huwezi kuajiri mtu wa kubeba ugonjwa na kufa kwa ajili yako.Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kupatikana wakati limepotea, "maisha".

Tukiwa katika hatua yoyote ya maisha, baada ya muda tutakabiliana na siku ambayo pazia litafungwa mbele yetu. Penda familia yako, Mwenzi wako na marafiki. Watendee mema,watunze.

Kadiri tunavyozeeka na kuwa na hekima zaidi, tunatambua polepole kwamba kuvaa saa ya $300 au $30 zote mbili hutoa wakati mmoja.Tuwe na pochi ya $300 au mkoba au $30, kiasi ndani ni sawa.Tunaendesha gari la $150,000 au gari la $30,000, njia na umbali ni sawa, na tunafika mahali pale pale. Iwe nyumba tunayoishi ni futi za mraba 300 au 3000, upweke ni uleule. Kwa jinsi hiyo utatambua kwamba furaha yako ya kweli ya ndani haitokani na vitu vya kimwili vya ulimwengu huu,bali na Mungu.

Iwe unasafiri kwenye ndege daraja la kwanza au daraja la uchumi, ndege ikishuka, unashuka nayo. Kwa hiyo natumai unagundua kuwa unapokuwa sawa na Mungu, una marafiki, kaka na dada, ambao unazungumza nao, unacheka nao, unaimba nao, unazungumza juu ya kaskazini kusini na mashariki au mbingu na dunia hiyo ndio furaha ya kweli!

Huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri. Wafundishe kumjua Mungu, kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo, watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.

Maisha ni nini. Ili kuelewa maisha vizuri, kuna maeneo matatu:

~HOSPITALI
~ GEREZANI
~ KABURINI

Hospitalini utaelewa kuwa hakuna kitu bora kuliko AFYA.
Ukiwa gerezani, utaona kwamba uhuru ni kitu cha thamani sana.
Kwenye kaburi, utagundua kuwa maisha sio chochote.
Ardhi tunaokanyaga leo ndio paa letu la kesho.

Habari mbaya: tulikuja HATUNA kitu na tutaondoka bila KITU. Kwa hivyo tuwe wanyenyekevu kuanzia sasa na kumshukuru Mungu kwa YOTE.

Tafadhali peleka ujumbe huu kwa watu wengine, ili wajue kwamba Mungu anawapenda.

96% ya watu hawatapeleka ujumbe huu kwa wengine, lakini kama wewe ni mmoja wa 4% waliosalia, peleka ukweli huu kwa wengine. Mungu akubariki sana.
Story yako imenifanya nikumbuke kifo cha the late Safaricom Ceo, Bob collymore.
Alikuwa na kila kitu pamoja na pesa ndefu , when blood cancer took its toll , hakukuwa na namna ya kumfanya aeendelee kuishi!!!
Imagine top paid east african Ceo lying in his deathbed surrounded by famous and expesive doctors na hakuna yoyote anayeweza kuokoa uhai wake !.
Jamaa aliamuru akifa mwili wake uchomwe moto na ikawa hivyo.
 
You are very right.Biblia katika 1 Yohana 1:8-9 inasema hivi,
"8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 Bali tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki,hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Kwenye mambo ya dini uko vizuri, tofauti na na zile story zako za umbea kuhusu US.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Unexamined life is not worth living.
Hii phrase yako huwa naitafakari kila siku !! Honestly had we had choice before we were born , binafsi ,nisingechagua kuishi!!
I am realy struggling with the idea of life ,and whether it is worth living.
 
chamsingi ndugu zangu tutafute MUNGU napesa tu maana wengine hatuna nssf.mwenzako alikuwa anahela hata ya kumtibia ,jidanganye sasa
 
chamsingi ndugu zangu tutafute MUNGU napesa tu maana wengine hatuna nssf.mwenzako alikuwa anahela hata ya kumtibia ,jidanganye sasa
Huzuiwi Kuutafuta pesa mkuu,ila mtangulize Mungu kwanza in everything you do.Money without God ends you up in catastrophe,ruin and.sorrow.
 
Huu uzi unanikumbusha kuna mwamba mmoja umwambii kitu kuhusu kujenga japo anapesa ukimuuliza anakwambia awez kujenga safarini anasubili afike huko aendako kama ni mbinguni au ahera ndio atafanya ujenzi
Ha ha ha
 
formula ni moja tafuta hela na kula raha kama vile utaishi milele, fanya ibaada kila sekunde kama vile utakufa secunde inayofuata.
 
Lakini hata wewe sio mkamilifu mkuu.Kumbuka unapomnyooshea mwenzio kidole,vinne vinakuelekea wewe.Acha ufarisayo mkuu.

Biblia inasema katikà 1 Yohana 1:8
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 Bali tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
1. Ni kawaida wenye dhambi mkiambiwa muache dhambi mnakimbilia kusema mnahukumiwa.

2. Mnakimbilia kusema hakuna mkalifu, Biblia hiyo hiyo inasema 'Watakatifu waliopo duniani, ndio nnaopendezwa nao'.

3. Kama kuambiwa uache dhambi kisa unaona kila mru ni mdhambi unajidanganya na wahubiri wa injili waliofanya mpaka leo tumjue Kristo walifanya kazi bure, wale walikuwa ni watakatifu na dhambi haikuonekana kwao.

4. Usipendeke kutumia maandiko na kuyafafanua kwa utashi wako.
 
Back
Top Bottom