Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha

Maneno ya mwisho ya Steve Jobs, bilionea ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kuhusu maisha

Nimejifunza kwamba:
Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri. Wafundishe kumjua Mungu, kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo, watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Maneno ya hekima kabisa haya.
 
Cha ajabu zaidi ni dunia na jinsi tunavyoipenda,
Nipo zangu hapa naendelea na kibarua cha kumwaga Zege juu ghorofa ya 4,Jua linanichoma vizuri tu,faraja yangu ni kwasababu sipo peke yangu,tupo wengi,kazi na dawa stori kama zote za haki na zabatili,sidhani kama kuna anaewazakufa kati yetu na ninahakika sote tunakichukia kifo! kula yangu yakubahatisha,chumba cha kupanga hakina umeme wala maji,kigodoro changu cha futi tatu kwa sita,sina mke lakini nina mtoto wa nje,najitahidi kumuhudumia hata hivyo niwe mkweli sijaweza kumtimizia,nina wazazi wangu nawapenda na ninatamani kuwafanyia mengi mazuri,tayari nimetimiza umri wa miaka 36 sijawafanyia hiki wala kile japo bado ninamatumaini ipo siku nitawafanyia chochote cha kujifaharisha, si mvutaji wala si mlevi mie lakini nawezaje kujiepusha na tabia hizi ikiwa idadi kubwa ya washirika wangu niwatumiaji!?sipigi punyeto lakini tayari nimeshaanza kuona ugumu wa kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa na ikiwa pesa ya kuhonga mwanamke itakosekana italazimu kuwe na njia m'badala yakujiridhisha! huwa nawaza na kufikiria hivi "kifo"sio njia sahihi ya kupunzika!?shida kubwa ni kwamba hakuna nafasi ya majaribio katika hili vinginevyo ningejaribu.
Naam wale wenzangu namimi wenye chuki binafsi na kifo na huku maisha yamewaelemea basi natuendelee tu kupambana huenda nasi Mungu akatuona!
Ameeen.
 
Hii phrase yako huwa naitafakari kila siku !! Honestly had we had choice before we were born , binafsi ,nisingechagua kuishi!!
I am realy struggling with the idea of life ,and whether it is worth living.
Oooh i see, my friend, let take Arbert Camus stand then, life is absurd in short, and universe has no obligation to make any sense to you or to me. So you are nog supposed to searching for meaning of life your life should give meaning.

You should make your own meaning and not depend on meaning provided by other or institution.
 
1. Ni kawaida wenye dhambi mkiambiwa muache dhambi mnakimbilia kusema mnahukumiwa.

2. Mnakimbilia kusema hakuna mkalifu, Biblia hiyo hiyo inasema 'Watakatifu waliopo duniani, ndio nnaopendezwa nao'.

3. Kama kuambiwa uache dhambi kisa unaona kila mru ni mdhambi unajidanganya na wahubiri wa injili waliofanya mpaka leo tumjue Kristo walifanya kazi bure, wale walikuwa ni watakatifu na dhambi haikuonekana kwao.

4. Usipendeke kutumia maandiko na kuyafafanua kwa utashi wako.
🤣🤣Wenye dhambi?
We huna dhambi mkuu?
Aliyekamilika ni mmoja tu
Hongera kwa kuwa mtakatifu duniani
 
1. Ni kawaida wenye dhambi mkiambiwa muache dhambi mnakimbilia kusema mnahukumiwa.

2. Mnakimbilia kusema hakuna mkalifu, Biblia hiyo hiyo inasema 'Watakatifu waliopo duniani, ndio nnaopendezwa nao'.

3. Kama kuambiwa uache dhambi kisa unaona kila mru ni mdhambi unajidanganya na wahubiri wa injili waliofanya mpaka leo tumjue Kristo walifanya kazi bure, wale walikuwa ni watakatifu na dhambi haikuonekana kwao.

4. Usipendeke kutumia maandiko na kuyafafanua kwa utashi wako.
Mkuu kwa taarifa yako mimi nimeokoka nampenda Bwana Yesu sana.Hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako katika uchanga wangu wa kiroho,ila Mungu alinionya.Aliniambia hivi kama wewe huna dhambi,mimi kama dhabihu hunihusu,na nilikufa bure Msalabani.Alinikumbusha na kuniambia unahesabiwa haki bure,ndio maana Mungu akikuangalia hakuoni wewe,anamuona Yesu badala yako.Alinielekeza nisome Warumi 7:15-25
Inasema,
"15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
Warumi 7:15

16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
Warumi 7:16

17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
Warumi 7:17

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
Warumi 7:18

19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
Warumi 7:19

20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Warumi 7:20

21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.
Warumi 7:21

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
Warumi 7:22

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
Warumi 7:23

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
Warumi 7:24

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Warumi 7:25"

Mkuu hii ndio hali ya mwanafunzi wa Bwana Yesu was kweli,na kama wewe contradiction hiyo huioni,basi wewe sio mwanafunzi wa kweli Bwana Yesu,unajidanganya.Mtume Paulo aliiona contradiction hiyo katika maisha yake,sasa hatukuelewi wewe mwenzetu.

Mkuu ukweli unabaki kwamba kama wewe humkosei Mungu,basi Bwana Yesu hakuhusu.Kumbuka kwamba sisi ni Wana wa Mungu,kwa hiyo kama Wana tutamkosea Baba Yetu,yaani Mungu,tunamkosjjambo la kufanya ni kurudi Kwake kwa toba,na Yeye kama Baba yupo tayari kutusamehe.
 
🤣🤣Wenye dhambi?
We huna dhambi mkuu?
Aliyekamilika ni mmoja tu
Hongera kwa kuwa mtakatifu duniani
Achana naye huyo mkuu,hajitambui.Infact hajui hata Neno la Mungu.Anachotaka ni kumrudisha Bwana Yesu Msalabani wakati kazi ya wokovu ameshaimaliza.Bwana Yesu alikuja kuokoa wenye dhambi,wa kwanza nikiwa mimi,yeye kama hana dhambi Bwana Yesu hamhusu,akae pembeni.
 
Shaggy .ft. Rayvon, Wimbo "Angel"

[emoji445]Life is one big party when you're still young, But who's gonna have your back when it's all done

It's all good when you're little, You have pure fun.[emoji445]
 
formula ni moja tafuta hela na kula raha kama vile utaishi milele, fanya ibaada kila sekunde kama vile utakufa secunde inayofuata.
Very illogical.Ila sikushangai wewe ni wa kizazi kipya,that is how they have made you to be, hamna kesho.You have just proved that they are successful in their endevour.Very sad indeed.
 
Very illogical.Ila sikushangai wewe ni wa kizazi kipya,that is how they have made you to be, hamna kesho.You have just proved that they are successful in their endevour.Very sad indeed.
Maisha ni incertain. Kufa ni lazima sema ndo haijulikani ndo maana unatakiwa kuishi hivyo.
 
Back
Top Bottom