Maneno ya Nchimbi hayana maana yoyote ile!

Maneno ya Nchimbi hayana maana yoyote ile!

swala la kupambana
inamaana ni kuipigania?

kama alivyosema wapo tayari kwa mchakato wa katiba mpya
je kwanini ipiganiwe/ipambaniwe?
 
swala la kupambana
inamaana ni kuipigania?

kama alivyosema wapo tayari kwa mchakato wa katiba mpya
je kwanini ipiganiwe/ipambaniwe?
 
Hata kichaa huwa anaongea Ukweli mkuu.
Akisema
1+2= 3
Anakuwa amejibu sahihi kabisa.

Kuna Muda saa mbovu huwa inaongea ukweli

Ema anasukuma kete vizuri sana kuelekea 2030
USIWAAMINI CCM.
USIWAAMINI CCM.
Kwamba maneno yake ni propaganda za 2030? Basi ni kweli hayana maana.
 
Uko sahihi ile ni MICHEZO, kitu ambacho raia wanatakiwa kujua linapokuja suala la kutafuta madaraka CCM hawana utani watakupa chambo huku ukiona ni chakula mwisho wa siku wanakuiingiza mjini. MIMI NI MWANA-CCM Nakuhakikishieni haya matamko mbona bado watakuja wengi sana kusema yale wanayoyataka wananchi na wengine wataanza kumpiga SAMIA waziwazi na kipindi hicho yote itakuwa ni script ya 2030 wakishapata kile wanachokitaka ndio basi tena.
 
Ukitaka kujikumbusha unafiki wa CCM kwenye mambo ya maridhiano rejea miafaka yote ya CCM Zanzibar na wapinzani. Mara zote yamekuwa ya uongo na ulaghai.
 
Ukitaka kufa kwa sonona utumie uwezo wako wa kufikiri kuwachambua hawa jamaa wa ccm. Wote wapo sawa kwa interests zao, they don't care mwananchi anapitia nyakati gani.
 
Naungana na wewe Mkuu na nakuheshimu sana ila mimi maoni yangu ni kwamba hata kama kweli anachosema anamaanisha bado suala la katiba daima litabaki kuwa ni mchakato yaani hakuna namna utasema fulani aonyeshe kwa vitendo ni process inahitaji muda maelewano na pesa…so mimi sitegemei nchimbi kufanya kitendo chochote kudhihirisha wapo tayari kwa katiba imagine tu NEMC wanataka kuwa mamlaka kamili miaka na miaka na kila mtu anaunga mkono mpaka nchimbi yuko nao ila haiwi sijui hizi nchi zetu zina shida gani
Sahii ccm lijapo jambo la kusuka mkeka wako vizuri , tujiulize , Mwenyekiti Uvccm mamlaka ya kumkemea nchimbi anayatoa wapi , ni mwendawazimu tu atakubali maneno ya nchimbi japo yapo na mantiki kwa kiasi flani.

Watanzania mpaka sasa wamevurugwa , na walioko juu wamevurugwa kinachotakiwa mpaka sasa kwa Taifa ni neema ya Mungu tu
 
hayana maana yoyote kwako na wenzio!
Ila kwa waliosoma "CUBA" yana maaana kubwa sana sana.
 
Yule na CCM ni chanda na pete, tangu kuzaliwa kwake mpaka umri huu ni mnufaika mzuri sana wa hicho chama watu wasitarajie kuwa "Yuda" kweli.

Mimi namuona muhuni tu, anakuja na hoja ya katiba mpya kupambaniwa kwenye wiki ambayo watu kadhaa wamefunguliwa kesi za ugaidi kwa kupambania hicho alichokisema. Mkuu upo sahihi maneno yake matamu ila matendo yake ni tofauti kabisa

Hajawahi toa kauli yoyote, kuhusu oktoba 29 leo eti ndio tumuamini ikiwa ni mnufaika wa yale mauaji, yamemuweka ofisini
 
Katiba mpya ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2030. Mheshimiwa Nchimbi kakumbushia agenda muhimu ya CCM kwa sasa ambayo ni katiba mpya. Anaposema watu wapiganie katiba mpya anamaanisha watu wapiganie utekelezaji wa ilani kwenye ishu ya katiba mpya.
 
Nadhani zimeshapita siku mbili sasa tokea Emmanuel Nchimbi [mimi simuiti makamu wa Rais kwa sababu hakuchaguliwa kushika hiyo nafasi] azungumzie mambo ya katiba mpya, uanaharakati, na mengineyo.

Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Katika huu muda wa siku hizi mbili nimeyafikiria kwa kina, upana, na urefu wa hayo aliyoyazungumza.

Kwa juu juu, aliyoyazungumza, ni maneno flani matamu matamu maana kazungumza yale ambayo wengi wetu tunataka kuyasikia.

Kwa sisi ambao huishi maisha kwa kutumia kanuni, maneno aliyoyazungumza Nchimbi hayana maana yoyote ile kwa sababu hayalingani na matendo yake na yale ya wenzake.

Baadhi yetu huwa tunaishi kwa kanuni ya ‘nionyeshe matendo yako kuliko vile ambavyo unaweza kunielezea kwa maneno pekee [show me better than you can tell me].

Huyu Nchimbi ni haramu. Hakuna mtu aliyemchagua awe makamu wa Rais.

Baada ya kuua maelfu ya Watanzania, yeye na mwenzake Samia wakakimbilia kujiapisha kwenye kambi ya jeshi huku wakijua kabisa kuwa hakuna aliyewapigia kura.

Hapo maana yake ni kwamba walipora madaraka.

Huyo Nchimbi mpaka leo hii hajawahi kusema chochote kuhusu maelfu ya Watanzania waliouwawa na serikali ya chama chao ili tu waendelee kukaa madarakani.


Kwa maneno hatujui anasimama wapi ila tukiangalia matendo yake tunajua pasipo na shaka kuwa anaunga mkono mauaji yaliyofanyika.

Mtu yeyote mwenye dhamiri iliyo safi hawezi kukaa kimya halafu kwa wakati huo huo akawa sehemu ya hao waliopora madaraka kwa kumwaga damu mpaka za watoto wadogo kabisa.

Nchimbi hajaonyesha kusikitishwa na hayo mauaji.

Hajaenda hata kwenye msiba mmoja wa hao watu waliouliwa.

Hajakemea mauaji ya watoto yaliyofanyika.

Hajatoa hata pole kwa yeyote yule aliyeondokewa na mpendwa wake hiyo siku ya Oktoba 29.

Kwa ufupi ni kajikausha kana kwamba hakuna kilichotokea siku hiyo.

Mtu mwenye akili timamu na mwenye nia ya dhati kabisa ya kutaka kuibadilisha Tanzania, utarukaje hayo mauaji na kuanza kuongelea mambo ya katiba mpya?

Watanzania tunawezaje kwenda kwenye mambo ya katiba mpya bila kuujua ukweli wa Oktoba 29, kuhakikisha kunakuwepo na uwajibikaji wa waliohusika akiwemo Samia, na kuazimia kuwa hayo hayatatokea tena?

Mimi siwezi kumpongeza Nchimbi kwa maneno matupu yasiyoendana na matendo ya kundi lake.

Show me better than you can tell me and we may talk.

Other than that, you can either go kick rocks or go pound sand somewhere…..
Aisee
 
Uko sahihi ile ni MICHEZO, kitu ambacho raia wanatakiwa kujua linapokuja suala la kutafuta madaraka CCM hawana utani watakupa chambo huku ukiona ni chakula mwisho wa siku wanakuiingiza mjini. MIMI NI MWANA-CCM Nakuhakikishieni haya matamko mbona bado watakuja wengi sana kusema yale wanayoyataka wananchi na wengine wataanza kumpiga SAMIA waziwazi na kipindi hicho yote itakuwa ni script ya 2030 wakishapata kile wanachokitaka ndio basi tena.
Kipi cha msingi kinachokufanya useme wewe ni Ccm ilihali unajuwa wazi hicho ni chama cha wauwaji?
Yani kinachokufanya uendelee kujiita mwanaccm ni kipi hasa?
 
Back
Top Bottom