GE2025 Maneno ya Polepole hayawasaidii Watanzania kwa sasa, ni unafiki

GE2025 Maneno ya Polepole hayawasaidii Watanzania kwa sasa, ni unafiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nimemaliza kumsikiliza pole pole naona taifa linaandaliwa vema kisaikolojia kujisimamia mwaka huu.

Nukuu za Pole pole.

1/ Mama ukichukua form na kugombea Urais utakuwa umetutukana watanzania wote.

2/Mama unataka kugombea na Salum Mwalimu wa chauma, Mama unataka kugombea na Mpina wa Act. Kweli mama unataka kugombea na hawa na moyo wako una amani kabisa?

3/ Kwani Act sisi ccm hatuijuhi? Pole pole anatufumbua macho na kututhibitishia jambo hapa kuhusu Act.

4/ Pole Pole anashauri mama amuachie Mh Lissu bila masharti aende kwenye familia yake. Kisha aitishe muafaka wa kitaifa kabla ya kuingia kwenye uchaguzi. Amesema vyombo vya dola vitajipanga kutokana na maamuzi ya wananchi ambao ndio wenye nchi. Hapa maana yake tume isituambie muda umekwisha. Kila jambo linawezekana waamuzi wa mwisho ni wananchi sio ratiba za serikali na vyombo vyake.

5/ Kuhusu Hayati magufuli sizumgumzii chochote kila mmoja ameelewa code za Pole pole.

6/ Kuhusu Ndugai na kobe wa uvvccm kupandishwa juu ya mti ili kumtukana Ndugai na kumlazimisha ajiuzulu pia sisemi.Mtu yule kutoka kundi la mtandao anayeogopeka na kutisha. Aliyekwenda Dodoma kwa Ndugai na kumwambia jiuzulu na kisha mzee akasema.Nimekosa mimi...Nimekosa sana..Nisameewe huyo naye simzungumzii.Pole pole Amesema kundi hilo linatisha sana.

Hamphrey Pole pole you made my day.

Chadema wako sawa tukatae wahuni kwanza ndipo twende kwenye uchaguzi.This is our country.

Wale mnaodharau msimamo wa chadema muwe na adabu mmeelewa sasa nchi iko wapi.

Wale mnaosema wana chadema wanamezwa na hoja za pole pole muwe na adabu.Huyu jamaa ametujengea nguvu ya mapambano leo kiasi kwamba tunaona kabisa huu ndio mwaka wa mabadiliko.

Kataa wahuni ponyesha Tanzania.
 
Mtoa haja acha zako Hakuna unafiki hapo ila wewe ndiye mnafiki unayeelewa anacho kisema na kujifanya huelewi. Anayosema yana tija kwa Taifa, CCM na vyombo. Ukiwa na kichwa sungwi huwezi kuelewa.
 
Mtoa haja acha zako Hakuna unafiki hapo ila wewe ndiye mnafiki unayeelewa anacho kisema na kujifanya huelewi. Anayosema yana tija kwa Taifa, CCM na vyombo. Ukiwa na kichwa sungwi huwezi kuelewa.
Kwa akili zako za kisoda huwezi ukaelewa kuwa polepole yuko kazini na ccm iko nyuma yake,ujinga wa waTz kama wewe mliowengi mmekufa mnasubiri kuzikwa na hii inatokana na kutofikiri nje ya boksi.

Hata lowasa,kingunge,sumaye,nk wamewahi kuucheza mchezo huu.

WATANZANIA siyo wa kuonewa huruma kwani 90% ni maiti kama wewe wenye akili ni 10% tusiojishughulisha na siasa au dini.
Mnabadilishiwa nyimbo na picha tu wanamuziki na walewale.
 
Mnafiki ni wewe mjinga na zombie. Sisi yanatusaidia mno. Hakika polepole ametutendea haki. Matapeli ya kijani yamejulikana sasa

Haya ingia barabarani ukawaguse hao kijani na u-cdm wako lakini ukweli utabaki palepale cdm ninyi ni wanafiki na bendera fuata upepo mnaoishi nyuma ya vivuli vyenu.

Yeye au ninyi kama ni mashujaa kweli jitokezeni kama hamjawa historia.

Mwanaume halisi duniani ni anayesimama peke yake na kujipigania pasipo woga na kutafuta kuungwa mkono ja upande mwingine kama wewe na manoya wenzio.
 
Vichwa sungwi upeo wao wa kuelewa ni mdogo sana. Mpaka wabustiwe na vitu fulani ndio wanaelewa.
 
Mtoa haja acha zako Hakuna unafiki hapo ila wewe ndiye mnafiki unayeelewa anacho kisema na kujifanya huelewi. Anayosema yana tija kwa Taifa, CCM na vyombo. Ukiwa na kichwa sungwi huwezi kuelewa.
Haya polepole kama anawasaidia mbona Samia kaxhukua fomu ya kugombea pamoja na makelele yake?amemfanya nini?
 
Asingeshinga hizo nyadhifa, haya anayoyasema leo angeyajulia wapi?
Ukishayajua yanatusaidia nini?.Hivi ikiwa mtu anafanya mambo mabaya alafu badae ndo anaibuka kujifanya hayafurai yanayofanywa na wenzake hiyo inatusidia nini kama taifa?.Ufumbuzi sio kufanya madudu alafu ugeuke kujifanya mwema maana sisi sio Mungu kwamba unatubu kwetu wakati huo kuna watu uliumiza ndugu zao,ufumbuzi ni kutokufanya mabaya kabisa na kutojifungamanisha kabisa na mabaya.Kumuunga mkono shetan aliyejigeuza malaika ni ujinga kama ujinga mwingine,once a devil is always a devil.
 
Kwa akili zako za kisoda huwezi ukaelewa kuwa polepole yuko kazini na ccm iko nyuma yake,ujinga wa waTz kama wewe mliowengi mmekufa mnasubiri kuzikwa na hii inatokana na kutofikiri nje ya boksi.

Hata lowasa,kingunge,sumaye,nk wamewahi kuucheza mchezo huu.

WATANZANIA siyo wa kuonewa huruma kwani 90% ni maiti kama wewe wenye akili ni 10% tusiojishughulisha na siasa au dini.
Mnabadilishiwa nyimbo na picha tu wanamuziki na walewale.
Baada ya miezi mitano polepole kusahaulika ataibuka tena mwingine kuwapiga porojo zakuwafariji yatajitokeza majinga kushangilia..Watu wanaongozwa na mihemko kuliko akili.
 
Ni kweli unayoongea ni to let bado miezi michache watu wachague raisi

Lakini pia ccm wanakuaga na Mbinu za ajabu sana unaweza Kuta kapewa kazi ya kuwapumbaza wapinzani
Sikufahamu, haunifahamu..
Lakini nina imani utakuwa umefanikiwa sana katika maisha yako kwa kiasi fulani..
UNA AKILI SANA,
ni wachache wanalifahamu hili.
 
Ukweli mchungu,
Hata chadema walifeli kwenye kugomea uchaguzi,hatuna cha kubadili sasa ni kuburuzwa 5 years
 
Kuitumikia kwake serikali na viongozi fisadi na akakubali kuteuliwa nyadhifa mbalimbali serikalini akiyajua yoooote haya na kukaa nayo kimya ni wazi alikuwa ananufaika na huo uozo!!

Nivyema akawashitaki wote anaowatuhumu kwa makosa yao siyo kuwatonesha vidonda watanzania ni uhuni.
Maneno ya HP ni yamhimu sana kwa sasa yanawafungua macho, masikio, na akili Watanzania wote na wanaandaliwa vyema kisaikolojia kuliko kushitukizwa.
 
Maneno ya HP ni yamhimu sana kwa sasa yanawafungua macho, masikio, na akili Watanzania wote na wanaandaliwa vyema kisaikolojia kuliko kushitukizwa.
Kila kitu kina hatua haya hayo ma eno yamewasaidia au kubadilisha nini kwa waTz kisaikolojia na kiakili hadi sasa kwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom