Abuka
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 248
- 242
Kwa masaa kadhaa nimetafakari uwezo mkubwa na busara alizonazo Mama yetu, Rais wetu, Mama wa Vitendo, Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali leo.
Rais Samia ametumia miezi 6 kuwasoma viongozi wasaidizi wake, miezi 6 Amiri Jeshi Mkuu mwenye mamlaka kamili hajatumia nguvu bali hekima kujua aina ya viongozi wanaomsaidia katika majukumu.
Yaani ni kama kuchezea Sharubu za Simba akiwa amekaa tu anakuangalia bila kukufanya kitu, hii imetokea Tanzania ni nadra sana kupata viongozi wenye utulivu namna hii.
Hiyo ni busara ya viwango vya juu sana, tunajua watu wakishapata dola wanatumia nguvu badala ya akili, wengi wanajikuta wamekurupuka au wameingizwa chaka. Hekima ya aina hii inatoka kwa Mungu pekee.
Muda wa majaribio umekwisha, sasa Kazi imeanza. Baragumu limelia ni muda wa kuzinduka. Rais Samia ametangaza rasmi kwa wateule wote kwamba tunaenda pamoja kwa wananchi, ni mwendo wa kuwahudumia kwa vitendo vikali badala ya maneno.
Wale waliolala usingizi, chonde chonde muamke sasa, Mama amesema vitendo vikali ni zoezi endelevu.
Hekima aliyokuwa nayo Mfalme Suleiman hakika hata leo inaishi.
Watanzania tujifunze kupitia tunu tulizopewa kama Rais Samia Suluhu Hassan.
Mungu aendelee kukulinda, tunakupenda Rais wetu.
#TwendePamoja na Rais Samia