Maneno ya wachambuzi mbalimbali kuhusu Yanga

kilwakivinje

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
6,184
Reaction score
9,407
• Shaffih Dauda: Yanga wana timu bora sana msimu huu.

• Edo Kumwembe: Yanga bado wana timu imara sana kwenye Ligi yetu, maingizo mapya kila mtu ameona, yule Yao apunguze kuwa serious.

• George Job: Yanga hawana uwanja wa nyumbani wala ugenini, wana timu nzuri sana ya kupata matokeo popote.

• Gilbert Kaze: Yanga wamefanya mpira unaonekana kuwa rahisi sana Ila uhalisia ni namna walivyo na wachezaji bora kikosini, ni timu tishio sana msimu huu.

• Kocha Moalin: Ukicheza na Yanga na ukamiliki mpira kwa dakika 1 unapaswa kujipongeza, Yanga wasipokuwa na mpira ni hatari sana, na wanapokuwa na mpira ni hawakamatiki.

(Video haina uhusiano na habari)
 
Pacome hajacheza.
Kibwana hajacheza.
Sure Boy Hajacheza
Faridi Mussa Hajacheza
Skudu Hajacheza.
Gift Hajacheza.
Mauya Hajacheza.

Bado wameshinda Goal tano, this can be the Biggest Squad ever happen in football history of africa.[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Yaani mwaka huu hiiiiiiiiiiiiiiiiiii in Sukuma's voice.....
 
Tangu soka la nchi hii lianze hakujawahi kutokea timu bora kama Yanga hii ya Gamondi wala Yanga ile ya Nabi.
 
Africa???[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kid what u talk about??
 
Sisi wengine si wachambuzi bali wapenda soka, tuwekeze kwenye vipaji na wanaoweza kundeleza hivyo vipaji na si kwenye ndumba, tuachane na uchawi, kurogana, kufanyiana hujuma zozote katika soka, kusiwepo na kuhonga marefa au baadhi ya wachezajai wa timu pinzani, sijui kamati ya roho mbaya au kamati ya ufundi zipe jina lolote lile hazina tija kwenye maendeleo ya soka letu. Na wachezaji wetu wacheze mpira wa kistaarabu na si mpira wa kuumizana na kumfanya mchezaji akae nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha. Viongozi waliyopewa dhamana ya kuongoza taasisi zetu za mpira wafanye kazi zao kwa nia ya kuendeleza soka na si kupendelea timu wanazozishabikia au kukandamiza timu wasizozipenda. Mkufunzi Gamondi ni kocha ambaye ataleta mageuzi makubwa kwenye soka letu la Tanzania, kwani kila timu sasa itakapocheza na Yanga itabidi wafanye juhudi kubwa za kimbinu, fitness za wachezaji kuhakikisha wanaweza kuwamudu Yanga kwa dakika 90.
 
Uje kuwaweka tena hapa. Mambo YAKIHARIBIKA. Soon, time will tell
 
Tukiweka ushabiki kando yanga wapo vizuri.
 
Tangu dunia ianze haijawahi kutokea timu kali kama hii hata ije brazil inalowa
 
Chukua wachezaji wote wa yanga walioachwa baada ya wenzao kwenda katika timu za taifa uone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…