Maneno yanayokosewa sana katika matumizi

Hapo kwenye aghalabu ndio kwenye shughuli,nimejaribu sana kuwarekebisha watu lakini wananikatalia hua nawashangaa sana!
 
Aya badala ya Haya
Amisi badala ya Hamisi
Abari badala ya Habari
 
Wanatumia wakilisha mahala pa wasilisha na kinyume chake

Pia onyesha mahala pa onesha.
Onesha imetokana na ona na onyesha imetokana na onya
 
ukiona hivyo jua hao wabara, hawajatokea kaskazini wala hawajatokea zenji. manake wazenji na wakaskazini hawachanganyi haya maneno, piga ua.
 
Ukata na ukwasi yanawachanganya sana,,ama kupata radhi|kukosa radhi ya wazazi.Wengi hutafsiri kinyume chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…