Ndoa ikishafikia mahali ambapo wanandoa wanatukanana matusi ya makuli basi jua hiyo si ndoa bali ni kijiwe tu. Mume au mke anastahili heshima na kuthaminiwa. Huwezi kumuita mke/mume mbwa,, takataka, malaya, huna akili, mpuuzi, njinga, etc halafu utegemee upendo tena. Kumbuka ubongo wa binadamu ni smaku hivyo maneno mabaya huwa hayabanduki kabisa. Tuelewe kuwa matendo mema kwa mwenzako yanahesabika kuwa ni wajibu na unapofanya baya moja tu linakumbukwa kuliko yale mema mengi uliyokwisha fanya. Na baya moja linaweza kufuta yale mema mengi na ndoa ikabakia tu ceremonial. Ndoa inatakiwa kulindwa na kuheshimika. Pia kwa wale wapenzi/wachumba nao hali ni ile ile. Achana na maneno au matendo mabaya kwa mwenza wako. Kidonda chake hakiponi haraka na kovu lake si rahisi sana kufutika hata kama utaomba usamaha. Watch out guys.