Manesi wa mtaa wanaweza kusaidia afya za raia kwa ukaribu zaidi

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
1,017
Reaction score
2,163
Wizara ya afya ni muhimu sana katika jamii. Jamii yenye afya njema ina uwezo wa kuwa na uchumi bora. Huduma za afya zikiwa karibu zaidi na wananchi inapunguza idadi ya wagonjwa ma hospitalini.

Kuna magonjwa sugu kama magonjwa ya moyo na kisukari, msongo wa mawazo na kadhalika. Wengi wa wagonjwa wanaolazwa hospital ni kutokana na kushindwa kukabiliana na magonjwa haya.

Nurse wa mtaa atajua wagonjwa wake, wale ambao wanashindwa kujichoma sindano za insulin, wanaotumia dawa za akili na magonjwa ya moyo, kuwapitia majumbani mwao kila siku asubuhi na kuhakikisha wamemeza dawa zao. Mchana awe kituoni mwake akiandika ripoti ya kila alichomfanyia kila mgonjwa. Pia kusafisha na kufunga vidonda. Wenye kisukari wengi wanaishi na madonda sugu.

Ripoti itasaidia wataalamu wengine kujua matibabu ya kila mgonjwa. Hata ikitokea siku nurse wa mtaa anaumwa atakae mpokea atajua kinachoendelea.

Nurse wa mtaa atoe elimu mtaani anapopata nafasi kuhusu matumizi ya pombe yaliyopitiliza na ngono zembe pia ulaji wa chakula bora na kufanya mazoezi. Mgonjwa anaporuhusiwa kutoka hospitali, kuwe na nakala ya barua kwa nurse wa mtaa kutoka kwa daktari kwa maelezo ya uwangalizi unaohitajika.
 
Halafu muda wao nani atawafidia .ikiwa tuu huko kwenye majukumu yao ya kila siku hawalipwi vizuri,mapunjo kibao,Qnet imewafanya vibaya uwaongezee stress tena na za mtaani.

Au labda unamaanisha serikali iajiri manesi wa mitaani?
 
Back
Top Bottom