Mange Kimambi ahojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798


Blogger Mange Kimambi wa u-turn Blog ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.

Polisi wamemkamata wakati ameenda kuchukua fomu ya kutia nia kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kwenye moja ya majimbo ya jiji la Dar.

Mpaka sasa yupo mikononi mwa Polisi akihojiwa kuhusu mienendo ya uendeshaji wa blogu yake na mitandao mingine ya kijamii.


Mange alipokwenda kuchukua fomu ya Ubunge wa jimbo la Ubungo kabla ya Kukamatwa na Kupelekwa Rumande


Mange akiingizwa Gari LA makachero kuelekea rumande


Akiwa ndani ya Gari jeusi kuelekea polisi

========
UPDATE - Julai 17, 2015

Mange Tayari ametoka kwa dhamana aliyowekewa na mtoto wa Mvungi muda mchache uliopita (05:15pm)



Kwa mujibu wa William Malecela, mpaka sasa Saa Tisa Kamili Mange alikuwa amemaliza kutoa maelezo ya awali na anakabiliwa na Kesi za wananchi 7 ambao tayari wameshamfungulia Mashitaka ya kudhalilishwa kwenye Blog yake.

Imebainika kuwa ana kesi ya mujibu wa Polisi Cybercrimes Unit, na huenda akawa na kesi ya kujibu kutoka Usalama wa Taifa na ana kesi ya Polisi wenyewe Oysterbay
 
Ebwanaeeeh! i expect this,huyu mama mpaka hapa kaisha, haiwezekani utukane watu halafu ujilete huku eti ni nchi yangu siogopi lolote! Angebaki USA tu. Pole mange zigo hilo mpaka ulitue!
 
Endelea kuongeza nyama!

Kwenye blog yake ameandika kuhusu kumreport Abdul (mume wa Shamim) kwa kutishia kumwua kwa bastola, taarifa iliandikwa jana kwenye blog, hivyo na assume kutishiwa na kureport ilikuwa jana pia.

Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba Abdul Nsembo alifanya tukio hilo Dar Free Market ambapo Mange alikuwa ameenda kuchil na marafiki zake. Kisa ni kwa sababu Mange anamwandika Shamim as Mrs Sembe!

Kama hiyo taarifa yako ni ya kweli, ukute jamaa amemzunguka kama vipi!
 
Free Mange Kimambi.

I am not a fan of Mange. I am a fan of Freedom of Speech.

This just elevates Mange beyond her current status.

Cc Nyani Ngabu

It most definitely does.

They are putting her on a pedestal on which she doesn't belong.

She has the right to be stupid and spew drivel on her blog.

But at the same time she can't be given carte blanche to libel people.
 
Ndio nani?

Juzi hapa alikuwa anamtukana Lowassa, Kingunge, January Makamba, Mke wa Mengi, Ridhiwani Kikwete na wengineo pia amekuwa akitukana watu yaani wananchi ovyo kwenye blog yake na pia kutoa masiri ya waliokuwa rafiki zake na za makampuni waliyofanyia kazi habari nyeti.


Jana kaleta habari ya kutishiwa na bunduki ila hatujasikia ya upande wa pili wala mashaidi so inasadikiwa na chumvi kaongezea katika maelezo yake.
Duh
 
No no.......free our Mange pls........hope sio kweli.......
 
hapo vikwazo vitaihusu serikali,uhuru wa kutoa maoni utakua umekiukwa.....
 
Akitoka atatueleza kwenye mitandao kilichojiri as amesema lazima apambane na watu wanaopindisha makona.
 
Jana, alifikia Kituo cha Polisi Oysterbay kuripoti tukio la yeye kutishiwa Bastola hadharani na Abdul Nsembo, mume wa Shamimu wa 80/20 Fashion Blog..

Movie ndio kwanza imeanza..

View attachment 268670
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…