mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798

Blogger Mange Kimambi wa u-turn Blog ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.
Polisi wamemkamata wakati ameenda kuchukua fomu ya kutia nia kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kwenye moja ya majimbo ya jiji la Dar.
Mpaka sasa yupo mikononi mwa Polisi akihojiwa kuhusu mienendo ya uendeshaji wa blogu yake na mitandao mingine ya kijamii.
Mange alipokwenda kuchukua fomu ya Ubunge wa jimbo la Ubungo kabla ya Kukamatwa na Kupelekwa Rumande

Mange akiingizwa Gari LA makachero kuelekea rumande

Akiwa ndani ya Gari jeusi kuelekea polisi
========
UPDATE - Julai 17, 2015
Mange Tayari ametoka kwa dhamana aliyowekewa na mtoto wa Mvungi muda mchache uliopita (05:15pm)
Kwa mujibu wa William Malecela, mpaka sasa Saa Tisa Kamili Mange alikuwa amemaliza kutoa maelezo ya awali na anakabiliwa na Kesi za wananchi 7 ambao tayari wameshamfungulia Mashitaka ya kudhalilishwa kwenye Blog yake.
Imebainika kuwa ana kesi ya mujibu wa Polisi Cybercrimes Unit, na huenda akawa na kesi ya kujibu kutoka Usalama wa Taifa na ana kesi ya Polisi wenyewe Oysterbay