kazuramimba
Senior Member
- Jun 14, 2011
- 145
- 154
Lema amepotoka sana. He’s on the wrong side na hana ujanja wa kushinda hii ligi. He’ll become politically bankrupt before he knows it!Kutoka jijini Los Angeles huko Marekani, Mwanaharakati na Dada wa Taifa Mange Kimambi amemjibu Godbless Lema ambaye anadaiwa kulamba asali na kutuhumiwa mitandaoni kwa usaliti.
Ameanza kwa kusema Moja ya vitu Chadema imejijengea katika jamii ni kwamba wanapigamia utawala wa Sheria. Kwamba wanapigania HAKI, Ila Lema kwenye PRESS yake ya Jana ni wazi ameona ni vyema apitie njia za PANYA. Njia za kupigiana simu na kuongea na wakubwa fulani. Njia za kuomba huruma kwa wauwaji, njia za Kuwapigia magoti watekaji, Serekali haramu.
Mange ameendelea kusema LISSU yuko ndani mpaka sasa hivi kwasababu anapigania utawala wa Sheria. Angetaka kutoka kwa huruma za watu angeshatoka Kitambo sana.
Mange ameenda mbali na amekumbushia kuwa Mbowe ambaye aliingia JELA na Mbowe aliyetoka jela walikuwa ni watu tofauti kabisa kwa Sababu alitoka Jela kwa huruma za Samia Suluhu ndiyo maana alipotoka akaamua kuiuza CHADEMA, gafla akaanza kuimba mapambio.
Akaendelea kusema kuwa LEMA anataka LISSU naye atoke jela kwa huruma za Samia ili naye akauze CHADEMA.
Mange ameendelea kusema LEMA ameshafika bei, sasa anajaribu kuimaliza CHADEMA.
Kwa uchungu mkubwa Mange ameendelea kusema Abdul anamdharau LEMA kupita kawaida, anamuona LEMA ni mshamba na poyoyo hasa baada ya kutetemeka alipopewa maburungutu ya pesa za damu. Mange amedai pamoja na Lema kumtusi na kumuita Mpumbavu bado heshima yake iko pale pale na kwamba Abdul ana muheshimu yeye Mange kimambi kupita kawaida. MANGE amedai Abdul alivyomfuata huko Marekani aligoma kuhongwa, alisimama kidete ila LEMA kanunulika.
Amedai kuwa LEMA akiziona hela za Abdul anatetemeka mpaka Abdul anamuona mshamba, anamcheka na kumuona popompo. Mange amedai kuwa Abdul ambaye ameishia darasa la nne amemteka LEMA kiakili kiasi LEMA amekuwa poyoyo. Kile ambacho Lema anaita ni Strategic Engagement ni janja tu maana ameshafika bei.
My take: Mange ameacha maswali ya msingi sana.
Je, imekuwaje chama kinachodai haki na sheria, mmoja wa viongozi wake anaenda kuomba huruma kwa wale wale wanaotakiwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria?
Basi watu watafakari, wakisema: Je, haki hudaiwa kwa sheria, au hutegemea huruma ya wenye mamlaka?
Chadema ni chama cha demokrasia nadhani kila mtu aruhusiwe kuwa na maoni yake kila chama kina wahafidhina, waliberali na moderates maana wote hamuwezi kuwa na mtazamo sawa. So kama lema kakosea atahukumiwa na kamati kuu na sio kwingine.
Na kuhusu Mange aisee sielewi kwanini anapewa attention kiasi hiki, amekua kama msemaji wa Lissu na chadema kitu ambacho sio sawa. Ana haki ya kutoa maoni yake ila asiwe ndio chanzo cha kuaminika hadi kufikia stage chama kinataka kupasuka kisa mwanaharakati aliye nyuma ya keyboard.
Chama kinaendeshwa na vikao sio tweets za Mange. Chadema iheshimiwe na wote akiwemo Lema na Mange otherwise wasitutoe kwenye reli maana hii wiki ni ya muhimu zaidi pengine kuliko zote katika historia ya chadema I tunaishia kujadili Mange this Mange that.
My two cents.....
ila wewe, unamhemuko sana.Mange nonsense...
- Lema anadharauliwa sana na Abdul... ooh mimi Mange Abdul ananiheshimu sana..!
Hiyo heshima anayodai kupewa na Abdul yeye alijuaje kama anapewa?
Nae huwa anaongea na Abdul kwa simu sio!.
- Lema alipowekewa maburungutu ya pesa alitetemeka!, alikuwepo akamuona Lema akitetemeka?!
Anaishi kwa habari za kuambiwa kisha anaziamini kwa 100% then anataka na wengine tuziamini kama anavyoziamini yeye!
Kila siku ushahidi hana, ni kelele tu, ndio maana akipingwa anatishia kuwasemea wengine ili wafukuzwe U.S.
Kuwa mfuasi wa hiki kiumbe lazima uwe mjinga kama chenyewe, Lema aache kuhangaika na hii akili ndogo anapoteza muda.
Utakuwa mfuasi wa Mange, usinipe kazi ya kuutafuta umbea!.ila wewe, unamhemuko sana.
Kamsikilize tena Mange akujibu hoja zako.
soon tutamuona kwenye kila uzinduzi na kuhani misiba kama kaka yake.Nilisema mimi naona dada wa taifa kagongelea msumari..!!
Wewe ndio un atakiwa umsikilize akujibu. maana maswali yako umeshayajibu. Sijui umepewa stori.?Utakuwa mfuasi wa Mange, usinipe kazi ya kuutafuta umbea!.
Hiko ndo kinachofata, kajivunjia heshima ya miaka yote aliyoitengeneza..!!soon tutamuona kwenye kila uzinduzi na kuhani misiba kama kaka yake.
Huyu kishawekwa kwenye mshikaki mmoja na Kabwe Zuberi.Lema amepotoka sana. He’s on the wrong side na hana ujanja wa kushinda hii ligi. He’ll become politically bankrupt before he knows it!
Ndio ninachokiona hapa hawa inawezekana wanajuana wenyewe kwenye mambo yao mengine nje ya ChademaKwamba Abduli alimfata Mange Usa halafu mange hakukubali kununulika? Ila walionana!
Kwamba Abduli anamdharau sana Lema ila anamheshimu sana Mange?
Hawa mbona kama wote wanapambania maslahi yao!