Mange Kimambi amtupia kijembe Hamisa.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Urafiki wa kinafiki kati ya Mange Kimambi na Hamisa Mobeto unazidi kutia mashaka kila kukicha.

Mobeto amekuwa akimtupia vijembe vya chinichini Mange Kimambi katika hali ya kuigiza kama utani, pia Mange amekuwa akimtupia vijembe Hamisa lakini akiulizwa huwa anaruka futi mia na kudai hajamlenga Hamisa hata kidogo.

Hapo namba tisa Mange amemtupia kijembe Hamisa kwamba anajifanya anamaisha mazuri kumbe anafake tu maisha.

Hamisa Mobeto tangu kodi ya nyumba iishe amekuwa mtu wa kuhangaika huku na kule kuwapigia simu wazazi wenzake,Diamond na Majizo wamsaidie angalau kodi ya nyumba kwa sababu anateseka na watoto, na mbaya zaidi Hamisa muda mwingine anapiga simu mpaka usiku wa manane kumbembeleza Diamond Platnumz warudiane kitu ambacho kinamkera sana Mange Kimambi.

Kwa kifupi Mange Kimambi anampenda sana Diamond Platnumz kuliko kawaida ila anashindwa amuanzie wapi ndiyo maana kila mtu ambaye anadate na Diamond ,Mange huanza kumchukia tu bila sababu kwa sababu anatamani nafasi hiyo angepata yeye.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi hujiuliza hivi Hance Mtanashati ni mwanaume wa mikoani? Mwanaume wa dar? Mwanaume wa Pwani?.
Mada zako siku hizi mmhh.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…