Mangi aingizwa cha jiji

Dah! Mangi amewaaibisha sana Mangi wenzake duniani kote.
 
Ila mshana daaah
 
Ila mshana
 
Wanaokaa Manzese - Bakhressa njia ya kwenda tandale kituo cha polisi Kuna nyumba ya wageni inaitwa New York,nyuma yake kulikuwa na Mzee wa kingoni alijenga nyumba yake nzuri sana,enzi hizo mapambano yote ya Tyson tulikuwa tunaangalia kwake,Mzee pekee aliyekuwa na TV mtaani kwetu.
Mzee Bambo alikuwa dereva wa malori wa kampuni ya bia (TBL) Mungu alimjaalia maisha mazuri sana kipindi hicho cha 1990's Mtoto wake alikuwa anasoma sekondari ya St. Anthony ya mbagala.

Baada ya miaka kadhaa hali ya kimaisha ilibadilika kazini aliondolewa akawa anaenda bandarini na kupata kazi za kupeleka gari za 'IT' nchi za jirani.Sasa katika kipindi hicho alikutana na hao waganga matapeli wakamuahidi atapata pesa nyingi na atanunua ghorofa maeneo ya magomeni,Mzee bambo hakuwa na pesa za kutosha kuwalipa akaamua auze nyumba yake,kabla ya kuiuza vikao vya kifamilia vilifanyika ili kumzuia Mzee Bambo asiuze hiyo nyumba,mabishano makali sana yalitokea Mzee aliamua kuuza nyumba yake na kuwakabidhi wale waganga kiasi chote cha pesa kilichopatikana.

Baada ya hapo waganga walitokomea kusikojulikana Mzee alibaki na sanduku lake, baada ya siku kadhaa kupitia Mzee alifungua sanduku kilichofuatia ni kilio na kuchanganyikiwa,Mzee alipata ugonjwa wa moyo na akili yake haikuwa sawa.

Akaenda kupanga maeneo ya njia ya uzuri baada ya miaka kadhaa Mzee bambo alirudi kwao Ruvuma na umauti ulimkuta huko.
 
(Mkuu umetaja maeneo yangu ya kujidai nilipokuwa mdogo, mimi makuzi yangu nimekulia nyuma ya Hotel ya Mexico City kwa sasa wanapaita Discpline kitengo)

Matapeli wengi wa aina hii ya utapeli walikuwa maskani yao ni Manzese, mbinu yao kubwa ilikuwa wakikuona una ukaribu na mtu mwenye uwezo kiuchumi wanakurubuni wewe ili wamtapeli huyo mtu.
Mbinu nyingine wanatapeli wale watu waliokuwa vizuri kiuchumi halafu wakayumba wanawaambia kuna jini lichukua pesa zako na utaonyeshwa kwenye sanduku kabisa. Jinsi ya kuzipata mchakato wake ndio kutapeliwa kunapoanza.
Utapeli huu ulivuma sana miaka ya 2000's nashangaa huyu jamaa ametapeliwa kwa mbinu ya kizamani sana.
 
Maeneo ya.wazazi wangu hayo nilizaliwa na kukulia huko,bila shaka utakuwa unawafahamu akina bakari manjenga,yahaya Maliki,Mzee kichanga,Mwalami likonda,Ngade,marehemu roja mjeshi,mchodo,mokili,Babu Alex......
Displine kitengo napafahamu vizuri sana
 
Kumbe utajiri wa uganga umehama kutoka nyanda za juu kusini hadi kwa wezi wachaga?
 
Niliwahi kupanga kwa mstaafu wa jeshi kule Mtoni kwa Aziz Ally nyuma ya Sabasaba karibu na uwanja wa Sifa, huyu mzee naye alitapeliwa na wanaijeria na kuuza hiyo nyumba yake.. Alikufa ndani ya mwaka mmoja baada ya huo utapeli
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…