Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
 
..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
Mwalimu Nyerere alipendekeza kuwa yuko tayari Tanganyika tuchelewe kupata uhuru kwa sababu za Uumajumui wa Pan Africanism ili tuwasubiri wenzetu wawe tayari tupate uhuru kwa pamoja na kuungana na sio kwa sababu hatukuwa tayari, lakini hoja ya Mangi Mkuu ilikuwa ni Northern Province ndio ipewe uhuru kwanza kwa sababu tayari walikuwa well developed.
P
 
Mohamed Said,

..ungetusaidia sana hapa JF kama ungetupatia hotuba ya Mangi Marealle aliyoitoa UN.
JK,
Nami naitafuta.
Mtoto wa I. C. Chopra katika ujumbe ule wa Chief Marealle aliniomba nimsaidie kupata taarifa za baba yake safari ya UNO sikufanikiwa.

Ujumbe ule ulikuwa na watu hawa: I.C. Chopra, Sir Charles Phillips na Yustino Mponda.
 
P,
Nasubiri, ''maurongo,'' yangu nijikoshe tope ulilonipaka.
 
Usisome review, soma kitu original..... Reviews zinakuja baada ya kusoma kitu halisi
Yericko,
Ikiwa hakuna ''review, usione haya wala kujisikia vibaya kunieleza si lazima kila kitabu kifanyiwe pitiio na hiki chako hakitakuwa cha kwanza kukosa ''review.''
 
P,
Sawa kaka.
 
..nazungumzia kabla ya masuala ya umajumui wa afrika.

..pia kuna taarifa kwamba Marealle alisema mambo tofauti na hayo unayodai.

..pia katika Tanu kulikuwepo na watu prominent kutoka north province.

..vilevile Marealle na Umangi ulianza kupingwa na wananchi mbalimbali na harakati hizo ziliongozwa na vijana waliotokea Makerere na vyuo mbalimbali.
 
P,
Nasubiri, ''maurongo,'' yangu nijikoshe tope ulilonipaka.
Mkuu Maalim Dr. Mohammed Said, mimi siku zote najinasibu ni mkweli daima, nilichokisema kuhusu yale maurongo yako, naamini kabisa hata wewe kwa akili yako unajua yalikuwa maurongo ila uliyasema kwa malengo fulani, na excuse uliotoa kuwa maurongo hayo umeyapata wapi na kunipa reference, nitayatafuta nikithibitisha nitakusafisha, ila pia uwe mkweli, katika kuyazungumzia maurongo yako katika bandiko hili,

asilimia kubwa nimekutetea na kukufagilia. Asilimia ndogo tuu ndio nimekueleza ukweli wa maurongo yako na wala sii kiasi cha kukupaka tope, ni utando tuu wa bui bui, ukitanduliwa taratibu kanzu yako itabaki safi nyeupe kama ilivyo.
P
 
..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
JK,
Katika mapendekezo yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommittee ambao wajumbe wake walikuwa Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia mapendekezo kwa Constitutional Development Committeea 1950 TAA ilipendekeza uchaguzi wa kura moja mtu mmoja na baada ya hapo uhuru utolewe baada ya miaka 13.

Kwa hiyo TAA walipendekeza uhuru utolewe mwaka wa 1963.
 
..asante.

..nikipata muda nitatafuta alichokisema John Illife.
 
Mimi binafsi sina deni kwa Sheikh Mohamed wala wewe , ulitaka niandike juu ya Mzee John Rupia na nikakujibu kuwa historia ya Mzee Rupia imeishaandikwa ukijisumbua kidogo tu utaipata kule nilikuelekeza!! Hakuna hata siku moja hatumpongezi pale anapostahili!!! He is doing a commendable job to his country!!!
 
Slim5,
Anaestahili pongezi huyu kijana aliyetafiti na kuiweka historia ya Chief Marealle mtandaoni tuisome.

Mimi advantage ni kuwa nilibahatika kusoma Nyaraka za Sykes basi ni hili tu.
Huyu kijana kapinda mgongo kufanya utafiti.

Nasi tunakufanyia kama ulivyomfanyia huyu kijana [ CRITIQUE HIS WORK] kwa kunyoosha pale ambapo usahihi zaidi unatakiwa!!!
 
Nasi tunakufanyia kama ulivyomfanyia huyu kijana [ CRITIQUE HIS WORK] kwa kunyoosha pale ambapo usahihi zaidi unatakiwa!!!
Ndinani,
Wala sina shida na hilo ndugu yangu wakati wowote una jambo unataka kunifunza nifunze kwani nitakuwa jana nilikuwa silijui leo nimelijua.

Mtume SAW katufunza anasema kapunjika yule siku yake ya jana ni sawa na ya leo.
 
Naweza pata link na mimi napate kumjua zaid marealle

Slim5,
Anaestahili pongezi huyu kijana aliyetafiti na kuiweka historia ya Chief Marealle mtandaoni tuisome.

Mimi advantage ni kuwa nilibahatika kusoma Nyaraka za Sykes basi ni hili tu.
Huyu kijana kapinda mgongo kufanya utafiti.
 
Ndinani,
Wala sina shida na hilo ndugu yangu wakati wowote una jambo unataka kunifunza nifunze kwani nitakuwa jana nilikuwa silijui leo nimelijua.

Mtume SAW katufunza anasema kapunjika yule siku yake ya jana ni sawa na ya leo.

Shukran!
 
Mkuu unastahili honorary doctorate tena from London school of Oriental Studies. Unanikumbusha sana the late Prof. Mazrui na Walter Rodney.
Watu kama wewe ni hazina kubwa sana hapa JF.
Kazi zako nimeziona hata kule Library of Congress!! Hats off mkuu!!
 
Sherrif,
Ahsante sana ndugu yangu lakini umenifananisha na walimu wangu ambao siwezi hata kuwabebea viatu vyao.

Nashukuru sana shukurani zote zinamstahiki Allah.

Attachments

  • MOHAMED SAID LIBRARY OF CONGRESS.JPG
    72 KB · Views: 3
  • MOHAMED SAID NA PROF. ALI MAZRUI.JPG
    7.2 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…