Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Hilo andiko la Mangi Mkuu, Chief Thomas Marealle, sijabahatika kulisoma, ila kuna taarifa ambazo hazina uthibitisho kuwa Mangi Mkuu aliwaambia Wakoloni wetu Waingereza kuwa Tanganyika bado haijawa tayari kujitawala, ila North Province ndio wako tayari, hivyo kuwaomba watoe uhuru kwa mafungu, North Province ndio ipewe uhuru kwanza. Taarifa hii ilipomfikia Nyerere, ali curse kuwa never on earth mtu wa huko anaweza kuwa rais wa JMT!, japo hizi ni hearsay tuu, lakini political trends, na political dynamics za siasa zetu, zina onyesha ni kweli kuna makabila fulani fulani hayatakiwa kutoa rais wa JMT, na ni kweli sasa kuna chuki fulani ya kichini chini dhidi ya makabila fulani fulani!, huwezi amini kuna mtu fulani who was high ranking member wa utawala uliopita yuko mahabusu huu ni mwaka wa 4!.

..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
 
..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
Mwalimu Nyerere alipendekeza kuwa yuko tayari Tanganyika tuchelewe kupata uhuru kwa sababu za Uumajumui wa Pan Africanism ili tuwasubiri wenzetu wawe tayari tupate uhuru kwa pamoja na kuungana na sio kwa sababu hatukuwa tayari, lakini hoja ya Mangi Mkuu ilikuwa ni Northern Province ndio ipewe uhuru kwanza kwa sababu tayari walikuwa well developed.
P
 
Mohamed Said,

..ungetusaidia sana hapa JF kama ungetupatia hotuba ya Mangi Marealle aliyoitoa UN.
JK,
Nami naitafuta.
Mtoto wa I. C. Chopra katika ujumbe ule wa Chief Marealle aliniomba nimsaidie kupata taarifa za baba yake safari ya UNO sikufanikiwa.

Ujumbe ule ulikuwa na watu hawa: I.C. Chopra, Sir Charles Phillips na Yustino Mponda.
 
Mwalimu Nyerere alipendekeza kuwa yuko tayari Tanganyika tuchelewe kupata uhuru kwa sababu za Uumajumui wa Pan Africanism ili tuwasubiri wenzetu wawe tayari tupate uhuru kwa pamoja na kuungana na sio kwa sababu hatukuwa tayari, lakini hoja ya Mangi Mkuu ilikuwa ni Northern Province ndio ipewe uhuru kwanza kwa sababu tayari walikuwa well developed.
P
P,
Nasubiri, ''maurongo,'' yangu nijikoshe tope ulilonipaka.
 
Usisome review, soma kitu original..... Reviews zinakuja baada ya kusoma kitu halisi
Yericko,
Ikiwa hakuna ''review, usione haya wala kujisikia vibaya kunieleza si lazima kila kitabu kifanyiwe pitiio na hiki chako hakitakuwa cha kwanza kukosa ''review.''
 
Mkuu Maalim Mohammed Said, hatuna haja ya kuliharibu bandiko hili zuri la Mangi Mkuu, Chief Thomas Marealle, kwa kukumbushia yale maurongo ya nyuma.

Be at peace Maalim wetu, maurongo weka kando, sasa tuenende kwenye ukweli mtupu, tell only the truth and nothing else, but the truth and it is only the truth that will set you free from all the ill motives behind.

P.
P,
Sawa kaka.
 
Mwalimu Nyerere alipendekeza kuwa yuko tayari Tanganyika tuchelewe kupata uhuru kwa sababu za Uumajumui wa Pan Africanism ili tuwasubiri wenzetu wawe tayari tupate uhuru kwa pamoja na kuungana na sio kwa sababu hatukuwa tayari, lakini hoja ya Mangi Mkuu ilikuwa ni Northern Province ndio ipewe uhuru kwanza kwa sababu tayari walikuwa well developed.
P

..nazungumzia kabla ya masuala ya umajumui wa afrika.

..pia kuna taarifa kwamba Marealle alisema mambo tofauti na hayo unayodai.

..pia katika Tanu kulikuwepo na watu prominent kutoka north province.

..vilevile Marealle na Umangi ulianza kupingwa na wananchi mbalimbali na harakati hizo ziliongozwa na vijana waliotokea Makerere na vyuo mbalimbali.
 
P,
Nasubiri, ''maurongo,'' yangu nijikoshe tope ulilonipaka.
Mkuu Maalim Dr. Mohammed Said, mimi siku zote najinasibu ni mkweli daima, nilichokisema kuhusu yale maurongo yako, naamini kabisa hata wewe kwa akili yako unajua yalikuwa maurongo ila uliyasema kwa malengo fulani, na excuse uliotoa kuwa maurongo hayo umeyapata wapi na kunipa reference, nitayatafuta nikithibitisha nitakusafisha, ila pia uwe mkweli, katika kuyazungumzia maurongo yako katika bandiko hili,

asilimia kubwa nimekutetea na kukufagilia. Asilimia ndogo tuu ndio nimekueleza ukweli wa maurongo yako na wala sii kiasi cha kukupaka tope, ni utando tuu wa bui bui, ukitanduliwa taratibu kanzu yako itabaki safi nyeupe kama ilivyo.
P
 
..nadhani John Illife ameandika kuwa hata Mwalimu Nyerere mwanzoni alipendekeza Tanganyika ipate uhuru later than 1961. msimamo huo ulipingwa na wana Tanu ambao walitaka uhuru bila kucheleweshwa.
JK,
Katika mapendekezo yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommittee ambao wajumbe wake walikuwa Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia mapendekezo kwa Constitutional Development Committeea 1950 TAA ilipendekeza uchaguzi wa kura moja mtu mmoja na baada ya hapo uhuru utolewe baada ya miaka 13.

Kwa hiyo TAA walipendekeza uhuru utolewe mwaka wa 1963.
 
..asante.

..nikipata muda nitatafuta alichokisema John Illife.
 
Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Yericko Nyerere, Pascal Mayalla na juzi tu Ndinani.

Wote hao wana ahadi walizoahidi. Sasa ukishusha nondo namna hizi wanaona haya kutia lao, wataonekana, kwani ahadi ni deni. Lakini kwa uhakika wanakusoma.

Hawana njia bali wakubali tu kuwa wameshindwa kutimiza ahadi zao na wajitokeze tu. Japo wakupongeze tu panapostahili.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

"Wameingia mitini".

Mimi binafsi sina deni kwa Sheikh Mohamed wala wewe , ulitaka niandike juu ya Mzee John Rupia na nikakujibu kuwa historia ya Mzee Rupia imeishaandikwa ukijisumbua kidogo tu utaipata kule nilikuelekeza!! Hakuna hata siku moja hatumpongezi pale anapostahili!!! He is doing a commendable job to his country!!!
 
Slim5,
Anaestahili pongezi huyu kijana aliyetafiti na kuiweka historia ya Chief Marealle mtandaoni tuisome.

Mimi advantage ni kuwa nilibahatika kusoma Nyaraka za Sykes basi ni hili tu.
Huyu kijana kapinda mgongo kufanya utafiti.

Nasi tunakufanyia kama ulivyomfanyia huyu kijana [ CRITIQUE HIS WORK] kwa kunyoosha pale ambapo usahihi zaidi unatakiwa!!!
 
Nasi tunakufanyia kama ulivyomfanyia huyu kijana [ CRITIQUE HIS WORK] kwa kunyoosha pale ambapo usahihi zaidi unatakiwa!!!
Ndinani,
Wala sina shida na hilo ndugu yangu wakati wowote una jambo unataka kunifunza nifunze kwani nitakuwa jana nilikuwa silijui leo nimelijua.

Mtume SAW katufunza anasema kapunjika yule siku yake ya jana ni sawa na ya leo.
 
Mag 3,
Labda huenda umenisahau:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam.
  8. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  9. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  10. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  11. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  12. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  13. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  14. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  15. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  16. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  17. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  18. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  19. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  20. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  21. Awards: Several Awards
  22. Visiting Scholar: (2011)
  23. University of Iowa, Iowa City, USA
  24. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  25. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  26. OTHER COUNTRIES VISITED
  27. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

Mkuu unastahili honorary doctorate tena from London school of Oriental Studies. Unanikumbusha sana the late Prof. Mazrui na Walter Rodney.
Watu kama wewe ni hazina kubwa sana hapa JF.
Kazi zako nimeziona hata kule Library of Congress!! Hats off mkuu!!
 
Sherrif,
Ahsante sana ndugu yangu lakini umenifananisha na walimu wangu ambao siwezi hata kuwabebea viatu vyao.

Nashukuru sana shukurani zote zinamstahiki Allah.

Attachments

  • MOHAMED SAID LIBRARY OF CONGRESS.JPG
    MOHAMED SAID LIBRARY OF CONGRESS.JPG
    72 KB · Views: 3
  • MOHAMED SAID NA PROF. ALI MAZRUI.JPG
    MOHAMED SAID NA PROF. ALI MAZRUI.JPG
    7.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom