Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Mangi Mkuu Thomas Marealle katika nyaraka za Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kuna vijana naamini wamehamasika kutafiti na kuandika upya historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa kweli nawapongeza na nawatakia kila la kheri katika juhudi zao hizi.

Nimesoma makala moja ya Mangi Chief Thomas Marealle kwa bahati mbaya nimekuta kuna baadhi ya mambo mwandishi hakuyafanyaia utafiti wa kina.

Nimemwandikia baadhi ya mambo kama njia ya kumgutua na kumtia moyo:

''...katika hili bandiko la Chief Marealle kuna mambo unahitaji kuyapitia upya ili ipatikane ithibati ya ulichoandika.

Nimebahatika kumsoma Chief Marealle katika Nyaraka za Sykes barua binafsi ambazo akiandikiana na Ally Sykes.

Kwa ajili hii basi nimeweza kufahamu hata kile alichokuwa anakiamini ndani ya nafsi yake katika uongozi wa harakati za kudai uhuru.

Kuna barua moja Chief Marealle alikuwa anamuonya Ally Sykes kumtahadharisha na hali ya baadae baada ya uhuru.

Marealle alifika UNO lakini hakuwa mjumbe aliyetumwa kuwawakilisha Watanganyika.

Kuna jina moja umealiandika la mwanasheria kutoka Bermuda "Earl Seymour," naamini ulimkusudia Earle Seaton.

Earle Seaton pia nimekutananae ndani ya Nyaraka za Sykes akiwa mshauri wa TAA kuhusu "mandate territories."

Earle Seaton ana historia ya kutukuka katika harakati za uhuru wa Tanganyika hasa kwa TAA.

Abdul Sykes katika taatifa yake ya mwaka wa 1950 akiwa Katibu wa TAA kamtaja Seaton kama mtu aliyetoa msaada mkubwa kwa Constitutional Development Committee.

Abdul Sykes, Earle Seaton kama mwanasheria na Japhet Kirilo akiwa kiongozi wa Meru Citizens Union walifanya kazi pamoja kufikisha tatizo la Ardhi ya Wameru UNO 1952 na Kirilo akazungumza UNO Seaton akiwa mkalimani wake.

Yapo mengi.

Hotuba ya Mwalimu Nyerere UNO 1955 inatokana na waraka wa TAA Political Subcommittee ambao ndani ya waraka huu kuna mchango mkubwa wa Seaton.

Waraka huu ulijadiliwa mwaka wa 1954 katika kuasisi TANU na ni mapendekezo yaliyowasilishwa na TAA Political Subcommittee kwa Gavana Edward Francis Twining mwaka wa 1950.

Ningependa kukufahamisha pia kuwa Chief Marealle na Abdul Sykes walikuwa marafiki wakubwa.

Abdul akimtania Marealle akimwita, "King Tom," akimwambia Waingereza wanakataa kumwita yeye King ili asifanane na mfalme wao King George.

Mwaka wa 1951 Chief Marealle alichaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) Ally Sykes akiwa Katibu na Rashid Kawawa, Dr. Wilbard Mwanjisi, Michael Lugazia, Steven Mhando wakiwa katika Kamati.

Yapo mengi ningeweza kukueleza lakini nakuomba pitia upya historia ya Chief Marealle.''

EARLE SEATON NA JULIUS NYERERE.JPG

Earle Seaton na Julius Nyerere
 
Ahsante sana. Hakika unaitendea haki HISTORIA ya Tanganyika
Slim5,
Anaestahili pongezi huyu kijana aliyetafiti na kuiweka historia ya Chief Marealle mtandaoni tuisome.

Mimi advantage ni kuwa nilibahatika kusoma Nyaraka za Sykes basi ni hili tu.
Huyu kijana kapinda mgongo kufanya utafiti.
 
Huyu mzee baba Earle Seaton anastahili kumbukumbu... Be it a building, institution, street etc..
 
Vitu vya msingi kama hivi wachangiaji always ni wachache.

Sijui taifa la vijana tz linaelekea wapi.
Fizi...
Huko tulikotoka katika mada hii ilikuwa wachangiaji wakiingia hapa kwa ghadhabu kubwa wakati mwingine wakitukana na kutoa vitisho.

Hii ni kiasi cha kama miaka 10 iliyopita.
Lakini taratibu imewadhihirikia kuwa niandikayo ni kweli.

Hivi sasa somo limeeleweka kwa hiyo wachangiaji wamegeuka kuwa wasomaji wa kimya kimya.

Nina muda mrefu sijawaona Mag 3, Nguruvi na Mwanakijiji hapa ulingoni.

Hawa walikuwa wapinzani wangu wakubwa.
 
Kimolah,
Hakika Earle Seaton anastahili kukumbukwa.
Maalim Mohamed Said tunashukuru hata kwa kutupa hayo majina tu, tupate pa kuanzia.

Kama una nyaraka za Chief David Makwaia naomba tufanyie hisani uweke habari zake. Chief Makwaia na Chief Marealle walikuwa na sehemu kubwa sana katika mapambano ya uhuru tunaambiwa.
 
Mohamed Said ahsante sanaa.kama unaweza kutueleza kuna habari kwamba nyerere alipata upinzani mkubwa kutoka kwa wachaga wakati wa Uhuru kwamba wachaga walitaka kujiombea Uhuru kwa eneo lao tuu la Kilimanjaro sijui kuna ukweli kiasi gani kuhusu hili.

Shukranii.
 
Kiranga,
Sina nyaraka za Chief Kidaha lakini nina historia yake kupitia kumbukumbu za akina Sykes katika kipindi kile cha 1950s harakati za kudai uhuru zilipoanza.

Naingia Maktaba In Shaa Allah.

Attachments

  • CHIEF KIDAHA.jpg
    CHIEF KIDAHA.jpg
    132.9 KB · Views: 5
Mohamed Said ahsante sanaa.kama unaweza kutueleza kuna habari kwamba nyerere alipata upinzani mkubwa kutoka kwa wachaga wakati wa Uhuru kwamba wachaga walitaka kujiombea Uhuru kwa eneo lao tuu la Kilimanjaro sijui kuna ukweli kiasi gani kuhusu hili.

Shukranii.
Waterloo,
Hata mimi nimepata kusikia maneno kama hayo lakini maneno ya mtaani tu.
Sijapatapo kusoma historia hiyo popote.

Nimeandika kitabu, ''Uamuzi wa Busara,'' na muasisi wa TANU Kilimanjaro Mzee Yusuf Olotu alikuwa na msaada mkubwa kwangu lakini sikumsikia kusema lolote kuhusu shutuma hizi.

Nakuwekea hapa chini hali ya siasa ilivyokuwa Kilimanjaro wakati harakati za kudai uhuru zinaanza:

''Historia ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama walivyoshiriki wananchi wa Kilimanjaro, haiwezi kamwe kukamilika bila ya kutaja jina la Yusuf Ngozi.

Uchagga ilikuwa chini ya utawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi.

Baadhi ya machifu hawa walikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu na serikali ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza.

Hali ya siasa Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa. Wakati TANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umekwisha kwa wananchi kudhulumiwa haki yao. Japhet Kirilo alikuwa amerudi kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru mikono mitupu.

Kirilo hakuwa na chochote cha kuwaonyesha Watanganyika.

Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyeweza kuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo mjini akaieneza vijijini.

Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf ngozi ndipo unapokutana na historia za awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo; na wengine kuwa mawaziri katika Tanganyika huru, kama Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.

Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye pamoja na wazalendo wengine waliifanya TANU ishinde uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.

Kupitia kumbukumbu zake halikadhalika ndipo kwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe, mashujaa wa kike na wa kiume, wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, Amina Kinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika na wengineo.

Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawala wa machifu wao na kujiweka chini ya TANU.''

Hiyo paragraph ya mwisho inaeleza kila kitu.

Katika hali kama hii hao ambao inasemwa walitaka kudai uhuru wa Wachagga wangeanzia wapi?
 
Attachments

  • YUSUF OLOTU (2).jpg
    YUSUF OLOTU (2).jpg
    3.2 KB · Views: 3
Ahsante sanaa kaka kwa kunifundisha historia hii nimejifunza mambo ambayo sikuwahi kuyasoma darasani.
Waterloo,
Hata mimi nimepata kusikia maneno kama hayo lakini maneno ya mtaani tu.
Sijapatapo kusoma historia hiyo popote.

Nimeandika kitabu, ''Uamuzi wa Busara,'' na muasisi wa TANU Kilimanjaro Mzee Yusuf Olotu alikuwa na msaada mkubwa kwangu lakini sikumsikia kusema lolote kuhusu shutuma hizi.

Nakuwekea hapa chini hali ya siasa ilivyokuwa Kilimanjaro wakati harakati za kudai uhuru zinaanza:

''Historia ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama walivyoshiriki wananchi wa Kilimanjaro, haiwezi kamwe kukamilika bila ya kutaja jina la Yusuf Ngozi.

Uchagga ilikuwa chini ya utawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi.

Baadhi ya machifu hawa walikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu na serikali ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza.

Hali ya siasa Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa. Wakati TANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umekwisha kwa wananchi kudhulumiwa haki yao. Japhet Kirilo alikuwa amerudi kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru mikono mitupu.

Kirilo hakuwa na chochote cha kuwaonyesha Watanganyika.

Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyeweza kuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo mjini akaieneza vijijini.

Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf ngozi ndipo unapokutana na historia za awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo; na wengine kuwa mawaziri katika Tanganyika huru, kama Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.

Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye pamoja na wazalendo wengine waliifanya TANU ishinde uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.

Kupitia kumbukumbu zake halikadhalika ndipo kwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe, mashujaa wa kike na wa kiume, wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, Amina Kinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika na wengineo.

Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawala wa machifu wao na kujiweka chini ya TANU.''

Hiyo paragraph ya mwisho inaeleza kila kitu.

Katika hali kama hii hao ambao inasemwa walitaka kudai uhuru wa Wachagga wangeanzia wapi?
 
Fizi...
Huko tulikotoka katika mada hii ilikuwa wachangiaji wakiingia hapa kwa ghadhabu kubwa wakati mwingine wakitukana na kutoa vitisho.

Hii ni kiasi cha kama miaka 10 iliyopita.
Lakini taratibu imewadhihirikia kuwa niandikayo ni kweli.

Hivi sasa somo limeeleweka kwa hiyo wachangiaji wamegeuka kuwa wasomaji wa kimya kimya.

Nina muda mrefu sijawaona Mag 3, Nguruvi na Mwanakijiji hapa ulingoni.

Hawa walikuwa wapinzani wangu wakubwa.
Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Yericko Nyerere, Pascal Mayalla na juzi tu Ndinani.

Wote hao wana ahadi walizoahidi. Sasa ukishusha nondo namna hizi wanaona haya kutia lao, wataonekana, kwani ahadi ni deni. Lakini kwa uhakika wanakusoma.

Hawana njia bali wakubali tu kuwa wameshindwa kutimiza ahadi zao na wajitokeze tu. Japo wakupongeze tu panapostahili.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

"Wameingia mitini".
 
Back
Top Bottom