Mangungu ameshinda uchaguzi lakini wanachama wengi hawana furaha

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kitendo cha mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu kurud tena madarakani kwa miaka 4 tena kimepokewa kwa huzuni na masikitiko makubwa na wanachama wengi wa Simba, wengi hawakuridhishwa na uongozi wake hivyo wanaona miaka 4 mingine ni migumu sana.

Wengine tulishabaini kitambo sana tangu wakat wa kampeni kuwa Mangungu anaungwa mkono na Mo Dewji na wapambe wake, ilkuwa ngumu kumshinda kutokana na yaliyokuwa yakiendelea, alikuwa akipigiwa debe na akina Hassan Hassanoo mpiganaji ambao walikuwa wakifanya kampeni nje nje.

Nimejifunza kitu kimoja kutokana na uchaguzi wa jana.

1. Sasa hv wanachama hatuna tena thamani ndani ya Simba, ndio maana wengi tumelalamika uchaguzi namna ulivyoendeshwa.
2.Kaluwa ni mwanasheria msomi, amekataa kusaini matokeo kwa sababu anajua the election was not free and fair.
3.Mkae mkijua Mangungu anagombea ubunge kilwa kaskazini mwaka 2025, atakuwa busy sana kwenye siasa kuliko kuitumikia Simba.
4.Yanga wamefurahi kuona Mangungu amerudi kwenye uongozi
5.Uchaguzi haujakwisha, subirini mechi na Singida mtaona matokeo yake.
6.Hongera Mangungu, umewafanya wana Simba wajisikie huzuni kwa ushindi wako

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama mtu anaungwa mkono na mwekezaji wetu,Mo ndio kashinda kwanini hao mashabiki wasiwe na furaha na unajua fika Mo ni kipenzi cha wanasimba
 
Acha kuchanganya watu, wanachama wampigie kura then wana huzuni, hao wanachama ni mazuzu? Sema we ndio una huzuni kwani chaguo lako halijashinda. Kubali matokeo ndio ushindani.
 
Nikisema unasema uongo nitakuwa nasema uongo na Mimi. Ukweli uko wazi. Hadi Manzoki analetwa kupiga kampeni Uchaguzi ulidhaminiwa na Mtu mzito.
 
Hivi kwa akili yako wananchi walikuwa wanamtaka injinia?
 
Reactions: BRN
mangungu ni yanga na amewekwa hapo na gsm
 
Kitendo cha mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu kurud tena madarakani kwa miaka 4 tena kimepokewa kwa huzuni na masikitiko makubwa na wanachama wengi wa Simba, wengi hawakuridhishwa na uongozi wake
Mangungu ameshinda kwa kuchaguliwa na wanachama wengi. Kushinda kwa Mangungu kumehuzunisha wanachama wengi. Mbona kama ujumbe unapingana wenyewe?
 
Reactions: BRN
Mbona kule Kidimbwini FC wananchi walikuwa wanamtaka Manji mara paaa wakaletewa Injia? Hilo hamlioni?
 
Yani Simba kila wachofanya/Ongea lazima waitaje Yanga!
 
Utafiti wako umeufanyia wapi ..?

Umechukua sampuli toka kwa wanachama wa sehemu zipi..?

ili kujua wanachama hawana furaha.
 
Asiekubali kushindwa. WanaSeMBe tushikamane.
Nyuki mmoja mmoja hawawezi kutengeneza asali, lakini wakishirikiana wanaweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…