Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imefikia uamuzi wa kusimamisha kwa muda masuala na matukio yote yaliyokuwa yakiendelea kuhusiana na Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, ili kutoa fursa kwa uongozi kuangazia maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Bodi kilichokaa jana, Agosti 3, 2026. Kupitia taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo Agosti 4, 2026, Bodi imeeleza kuwa katika kipindi hiki nguvu na jitihada zote zitajikita katika kushughulikia masuala muhimu ya usajili wa wachezaji, maandalizi ya tamasha la Simba Day, mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na maandalizi ya Ligi Kuu.
Soma > Magori: Kikao cha Bunju ni batili, haukuwa Mkutano Mkuu rasmi wa Simba
Uongozi wa klabu hiyo, kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori, na Makamu Mwenyekiti, Murtaza Mangungu, umetoa wito kwa kauli moja ukiwasihi wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kusimama pamoja na klabu yao. Bodi imesisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha klabu inapata mafanikio makubwa katika msimu huu mpya unaoanza hivi karibuni.