Iconoclastes
JF-Expert Member
- May 26, 2014
- 4,091
- 2,511
Afrika kupigana na ufisadi ni kazi ngumu sana, hata kama una uzalendo na utashi wa hali ya juu. Marais wote kabla hawajaingia kwenye uongozi wa nchi huwa kuna makada fulani ambao huwa wamegharamia shughuli yote. Chukulia Bongo kwa mfano, rais wao Magu huwa anaongea kwa ukali sana dhidi ya ufisadi, lakini mwenyewe alishasema hawezi kufukua makaburi (yaani ufisadi uliotendeka kabla yake), juzi gazeti fulani lilijaribu kutaja viongozi wa hapo awali likapigwa ban ya miaka miwili.
Ukimskliza Tundu Lissu anavyotaja ufisadi ulivyokithiri hadi leo pamoja na mikwara ya Magu hadi inakatisha tamaa.
Hata mimi pia huwa najitathmini, kweli haya mambo yananikera, yananiuma sana kuona jinsi pesa za uma inavyopunjwa na hawa. Lakini je,.......najitia tu kwenye kiatu cha huyu rais wetu....hivi kweli ningefanyaje?
Hawa mafisadi wote ndio walinisadia kwa hali na mali kupatia uadhifa huu, nikiwachukulia hatua, si huenda nikapoteza uungwaji mkono na watu wa eneo lao? Na je, si kuna wafuasi wao serikalini ambao huenda wakani- undermine kisiasa?
Nami nataka kushinda tena kwenye uchaguzi ujao. Ama kama nilichukua uongozi kupitia mapinduzi, huenda hawa walionisaidia wakanigeuka hata kuniua!
Haiwezekani!!!