Manipulation: Mbinu iliyotumika na CIA kukichukua kisiwa huko Ufilipino na Sakata la Sumu Ofisi za Chadema huko Mbeya.

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Kuelekea Vita kuu ya Pili ya Dunia Marekani alikuwa na uhitaji mkubwa sana wa visiwa katika Bara la Asia kwa ajili ya kujenga Kambi zake za kijeshi.Moja ya maeneo yaliyotambuliwa na Marekani ni visiwa vilivyopo karibu na Nchi ya Ufilipino.

Pamoja na kutumia mbinu zote kuwashawishi wakazi wa visiwa hivyo kuhama ili wajenge kambi zao za Kijeshi, Marekani hawakufanikiwa kutokana na upinzani mkubwa waliopata kutoka kwa wakazi visiwa hivyo.

Baada ya kutumia mbinu zote shirika la ujasusi la Marekani liliingia kazini. Moja ya jambo la kwanza walilolifanya ni kusoma historia ya eneo lile na kujua imani pamoja na mila na desturi za wakazi wa eneo hilo.

Katika kusoma historia ya eneo lile, Marekani walikuja kugundua kuwa kulikuwa na imani za wakazi wa eneo lile kuamini uwepo wa Viumbe wanaonyonya damu binadamu (Zombies) hivyo CIA waliamua kuandaa tukio ambalo litawafanya wakazi wa kisiwa hicho kuamini kuwa kuna Zombie ili waame katika kisiwa hicho na Jeshi la Marekani likichukue na kujenga Kambi ya Jeshi.

Siku moja usiku, maofisa wa CIA waliwateka wanakijiji watatu wa kisiwa hicho na kuwaua. Baada ya kuwaua waliwatoboa matundu mawili kwenye shingo zao alafu wakawaning'iniza miguu juu kichwa chini kwa masaa kadhaa. Baadae alfajir waliwafungua na kwenda kuwatupa barabara tofauti za kijiji kile cha kisiwani.


Asubuhi ilipofika, wakazi wa Kijiji kile waliikuta miili ya wanakijiji mwenzao ikiwa imekauka na alama za meno mawili shingoni. Ilizuka taharuki kubwa sana kwenye kijiji kile iliyopelekea Wakazi wa Kijiji/ kisiwa kile kuhama wakiamini kuwa Zombie amekuja kuwaua na kuwanyonya damu. Baada ya Wananchi wale kuhama Marekani alienda kujenga Kambi yake ya Kijeshi kwenye kisiwa hicho.

Tukio lile halina tofauti sana na tukio la kumwaga unga katika Ofisi za Chadema Mbeya lililofanywa na wajinga wa vyombo vya dola vya Tanzania katika Ofisi hizo ili kuzua taaruki kuwa Ofisi ile imemwagiwa sumu then kufanya wananchi wasikusanyike kwenye Ofisi hizo kuendeleza jitihada za kumdai Mdude Nyangali.

Ni bahati mbaya sana Manipulation haiwezi kufanya kazi Mungu akiwa kazini.

Wito wangu kwa Polisi, TISS na CCM, waonyesheni Wakazi wa Mbeya ulipo mwili wa kijana wao Mdude Nyangali ili wamzike kwa amani.

Lord denning
Mwanza
 
Hii hatari sana,uzi umeshiba sana,Mungu yupo kazini mkuu usiogope
 
CCM, Polisi na wajinga wao TISS hawana akili.
Polisi na TISS akili wanazo ila zashikiliwa.

Hiyo yawazuia kutenda kazi zao kwa mujibu wa kanuni na sheria zinoongoza idara hizo na katiba ya nchi.

Ila CCM wanachama wake wengi akili zao huazimana hivyo ni vigumu kujitambua.

Chadema nao watu wake akili zao zilikuwa zashikiliwa na Mbowe na genge lake na yeye ni mtoto wa mjini.

Kaja Tundu Lissu kawafanya wajitambue na kwa kufahamu hilo wale wa CCM wamerudishiana akili zao (kwa kiasi) na wamegundua athari za kuwaachia Chadema na NRNE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…