KERO Manispaa Kisiwani Zanzibar hawatendi haki ubomoaji unaoendelea pembezoni mwa barabara

KERO Manispaa Kisiwani Zanzibar hawatendi haki ubomoaji unaoendelea pembezoni mwa barabara

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
kumetokea vunja vunja barabarani kisiwani Zanzibar na kwa mujibu wa maelekezo ni kuwa manispaa walitakiwa waondoe vimeza vilivyopo nje tu ya maduka au katika maeneo ya umma.

Lakini wao kwa kutimia manguvu yao wanakuja kwenye maduka ya watu na kutoa hadi vipaa vya maduka na wakati hadi beacon za barabara tayari zimewekwa na watu kuruhusiwa.

Kibaya zaidi wanaangalia na mtu kwa sababu unaweza kuvunjiwa wewe lakini mwengine ambae vipaa vipo saizi moja wakakiacha kama kilivyo wanaangalia uwezo na status ya mtu.

Hii sio haki hata kidogo kwa sababu wanakiuka maelekezo ya Serikali hivyo natoa wito kwa Serikali kulishughulikia hili mara moja na pia mkuubwa manispaa aachie madaraka kwa kusababisha hasara kwa watu bila haki.
 
Hadi kisiwa pendwa mnabomolewa! Poleni sana. Mamlaka zitasikia kilio chenu.
 
Back
Top Bottom