Manispaa ya Morogoro imedhamiria kukabiliana na hali ya uharibifu wa mazingira

Manispaa ya Morogoro imedhamiria kukabiliana na hali ya uharibifu wa mazingira

Joined
Dec 7, 2020
Posts
10
Reaction score
1
Kata ya luhungo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, imedhamilia kukabiliana na Hali ya uharibifu wa mazingira ulioonekana kuikumba kata hiyo ikiwa ni kiongozi mwa kata nne (4) zinazotegemewa kwa uhifadhi wa vyanzo vya maji vinavyopeleka maji yake katika bwawa la Mindu lililopo katika Halmashauri ya manispaa ya Morogoro ambalo kwa asilimia sabino (70%) ya maji yanayoingia katika bwawa hilo ndiyo yanayotegemewa na wakazi wa Manispaa hiyo.

Afisa Mtendaji wa kata ya luhungo John Joseph amefafanua kuwa,Ofisi ya kata ya luhungo imeandaa progamu maalum ya upandaji wa miche ya miti zaidi ya laki moja (100,000) katika maeneo yote ya pembezoni mwa vyanzo vya maji vilivyopo katika kata hiyo.

Lengo la kupanda miche ya miti hiyo,ni kurejesha uoto asili wa maeneo yote yaliyoathirika kwa kukosa miti ambapo hali hiyo inapelekea kukauka kwa Maji yanayotiririka kutoka milimani kuelekea katika bwawa la mindu.

Aidha,kupandwa kwa miti hiyo,kutapelekea pia kurejesha hali ya uoto asili wa Morogoro uliokuwepo kipindi cha mipaka ya 1980 na hali hiyo ilipelekea kuupa umaarufu mkubwa sana Mji wa Morogoro kwa kuwa na kijani kibichi kisichokwisha ambapo watu wengi walitamani kuigusa ardhi ya Morogoro ili washuhudie/wajionee wenyewe juu ya ufahari na utajili huo wa Morogoro.

Kuanzisha kwa programu hiyo kumetokana pia na changamoto ya hali ya upungufu wa maji uliojitokeza mapema mwishoni mwa mwaka jana 2021,ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro pamoja na kamati ya ulinzi na usalama, walilazimika kufanya ziara mbalimbali katika Maeneo yote ya vyanzo vya Maji ili kubaini sababu ya kutokea kwa upungufu wa maji katika bwawa la mindu.

Tarehe 04.12.2021, Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe adv.Albert Msando alifanya ziara katika kata ya luhungo kwa lengo la kukagua Maeneo yote ya vyanzo vya maji,pamoja na kupanda miche ya miti katika eneo la pembezoni mwa bwawa la mindu.

Mhe. Mkuu wa wilaya alilazimika kufika juu ya milima katika mitaa ya mundu, kilala,na Mlulu ambako viliko vyanzo siku vya maji na kushuhudia uwepo wa uharibifu wa Misitu katika baadhi ya maeneo na kuelekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa kupanda miti katika maeneo hayo.

Kadharika, Mapema mwanzoni mwa mwaka January 15,2022 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe Adv. Albert Msando aliongoza timu ya wataalam mbalimbali kwenda wilayani lushoto mkoani Tanga kwa lengo la kujifunza namna walivyofanikiwa wanalushoto kutunza na kuhifadhi Mazingira na vyanzo vya maji katika maeneo ya Makazi ya watu,katika kikao cha makaribisho na majumlisho madogo baada ya ziara hiyo wilayani humo, aliziagiza mamlaka zote zilizopo ndani ya wilaya ya Morogoro kufanya mikakati inayoeleweka katika kuhakikisha Maeneo yote hasa yaliyo na vyanzo vya maji, kupandwa miti ikiwa ni pamoja na kuilinda, kuitunza na kuihifadhi,pia alieleza kuwa, zipo sheria ndogondogo zinazotuwezesha kulinda na kutunza misitu na mazingira zikatumike ili kuhakikisha tunarejesha history ya uoto asili uliokuwepo katika kipindi cha miaka ya 1980 katika milima ya Uluguru.

Aidha, sheria hizo zikatumike kudhibiti uchomaji wa misitu hovyo na kwamba Mkuu wa wilaya ya Morogoro alionyessha kusikitishwa sana na vitendo vya baadhi ya watu katika maeneo mengine kufanya uharibifu wa makusudi kwa kujinufaisha wao bila kujari hali ya athari zitokanazo na uharibifu huo.

Hivyo Ikiwa kata ya luhungo ni sehemu ya maeneo yaliyoonyesha kuathirika na hali ya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji,na ikiwa tayari serikali imetoa maagizo yanayopaswa kutekelezwa,Sisi kama kata ya luhungo Nikishirikiana na Maafisa wa andamizi wa idara na vitengo mbalimbali katika kata,nimeanzisha kampeini Maalum ya upandaji wa miche ya miti katika vyanzo vyote vya maji vilivyopo katika kata ya luhungo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali na chama cha mapinduzi, lakini pia ikiwa mtendaji kazi unaotokana na uwepo wa uhalisia wa hali inavyoonyesha.

Kampeini hiyo tunatarajia kufanyika kuanzia Tarehe 03,04 na 05,02,2022 ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe adv albert Msando.

Kauli mbiu ya kampeini hiyo ni LUHUNGO TUREJESHE KIJANI YA MWAKA 1980 KATIKA VYANZO MAJI.


20201209_094603.jpg
IMG-20211204-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom