KERO Manispaa ya Musoma inapandisha kodi za vibanda vya biashara kiholela

KERO Manispaa ya Musoma inapandisha kodi za vibanda vya biashara kiholela

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wafanyabiashara nilipangishwa na manispaa ya musoma tangu mwaka 2018. Tumekua tukifanya shughuli zetu na kolipa kodi stahiki bila shida hadi ilipofika mwaka 2023 changamoto za kupandisha kodi kila mwaka zikaanza.
  1. Mwaka 2022/2023 nililipa kodi tsh 528,000 kwa mwaka kulingana na mita za mraba za kibanda changu
  2. Mwaka 2023/2024 nililipa kodi tsh 528,012 kwa mwaka kulingana na mita za mraba za kibanda changu
  3. Mwaka 2024/2025 nililipa kodi tsh 844,812 kwa mwaka kulingana na mita za mraba za kibanda changu ambapo walipandisha kwa 7,227 kila mita ya mraba
  4. Sasa mwaka 2025/2026 wametoa tangazo la kupandisha tena kodi na kufanya mita ya mraba kuwa 12,000.
  5. Ukizingatia hawafanyi ukarabati wa uchakavu wa vibanda wala kufanya usafi wa mazingira wafanyabiashara ndio wanaogharamia gharama za usafi kuwalipa magereza.
PXL_20260717_125942830.jpg

PXL_20260717_125846737.jpg
 

Attachments

Back
Top Bottom