Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
Serikali na Manispaa ya Ubungo tunaomba fungeni vyoo vya Mbezi Kituoni.
Vile vyoo ni hatarishi kwa afya ya binadamu kwa kweli, nimeenda mchana nikafika kuona vyoo 3 vinaelea kinyesi kizito juu, yaani unafungua hiki kimejaa maji na kinyesi juu nenda kile nenda kingine same.
Haitoshi mazingira ni ya hatari, ukweli mkojo ulirudi ndani nikauliza ikabidi niende kule chini kwenye. Vituo vya Kigamboni.
Wapendwa katika bwana yaani inasikitisha sana pesa zinakusanywa milango ya bati imeshindwa kuwekwa hata bawaba kweli naangalia mtu anaushika mlango anausogeza pemben ndio atoke nje aisee.
Mmh Mkuu wa Wilaya ya Ubungo tunaombaa tusaidie Watanzania kujali afya zao.
Pengine pesa za marekebisho kubwa nashauri kwa wakati huu watu waende kule chini kwenye keep-left ya kwenda Kinyerezi na Kibamba kuna magorofa na vyoo vizuri sana.
Ukweli sikujuta kutoa Shilingi 500 na niliapa sitoingia tena na tena.
Kinachoniuma ni Watoto, kama wakubwa tumeshindwa kujisaidia Watoto wataweza kweli? Si magonjwa tu jamani jamani.
Mganga Mkuu nenda pale ukaangalie hali halisi uone mateso na roho za mauti via vyoo.
Kuona maboresho ya Vvyoo, bofya hapa ~ Marekebisho ya vyoo Stendi ya daladala Mbezi Luis yameanza kufanyika