DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Katika taarifa ya Halmashauri hiyo iliyotolewa zaidi ya kipindi cha Mwaka mmoja uliopita ilieleza kuwa walikuwa wametenga kiasi cha Tsh. Milioni 600 kwa ajili ya maboresho mbalimbali.
Nikiwa mmoja wa Wafanyabiashara kwenye soko hilo, nasema wazi lipo katika hali ambayo inaweka mashaka na wasiwasi juu ya uwajibikaji wa wasimamizi wa soko hilo pamoja na utekelezaji wa ahadi za maboresho zilizotolewa.
Kuna miundombinu ya mitaro ambayo ilijengwa lakini katika hali ya kushangaza mitaro hiyo imejaa taka na kupelekea mvua zinaponyesha maji hayatembei ipasavyo, mitaro hiyo haisafishwi mara kwa mara na ikitokea wameisafisha uchafu unatolewa na kurushwa pembeni, mvua zikinyesha unarejea tena.
Soko hilo limekuwa likitumika watu wengi na sasa inaonesha tumekubali kuishi hivyo, lakini mazingira yake yanahatarisha sana afya zetu kutokana na uchafu ambao unaweza kuibua magonjwa.
Kwa kuzingatia taarifa ya Halmashauri iliyoeleza kuwa soko hilo linaingiza fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 1.2 kwa mwaka, naona sababu ya kuhoji, kwanini mamlaka zinasita kuona umuhimu wa haraka kuendelea kuboresha soko hilo, tulitegemea maboresho yangekuwa endelevu ili kuhakikisha mazingira yanakuwa rafiki, lakini hakuna dalili hizo tunaendelea kuteseka.
Wito wangu kwa Viongozi wa Wizara ya TAMISEMI, wafuatilie changamoto hii na kuweka msisitizo wa kuhakikisha mazingira ya soko hilo yanaboreshwa zaidi, hasa kwenye miundombinu ya ndani ambako wafanyabiashara tunapanga bidhaa, lakini ni vyema miundombinu ambayo imeshajengwa au kukarabatiwa hususani mitaro ikatunzwa kwa kuondoa uchafu mara kwa mara ili kuepuka kero wakati mvua zinaponyesha.
=============================
TUJIKUMBUSHE ILIVYOKUWA....