Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam Wakuu,
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums kudai kuna Utiririsha wa Maji taka kwenye Mitaro ya Ubungo Riverside, Manispaa ya Ubungo imetolea ufafanuzi.
Hapa chini ni Ufafanuzi;
"Ufafanuzi kuhusu uwepo wa mazingira hatarishi ya magonjwa ya mlipuko kutokana na utiririshaji wa maji ovyo wa majitaka ya vyoo eneo la Ubungo Riverside
Ufafanuzi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakiri uwepo wa maji taka katika eneo la Ubungo Riverside ambayo yametokana na kuziba kwa mitaro na shughuli mbalimbali za biashara katika eneo hilo ikiwemo Mabucha ya samaki wabichi na mama na baba lishe pamoja utupaji wa taka ovyo kwenye mitaro na hivyo kupelekea maji kutuama kwenye mitaro.
Baada ya kupokea kero hiyo, Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na Wafanyabiashara, Uongozi wa Serikali ya Mtaa wamefanya usafi katika eneo hilo ikiwemo kuzibua mitaro ili kuweka mazingira safi katika eneo hilo na hivyo kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Vilevile, ili kuwa na suluhisho la kudumu la usafi katika eneo hilo, Manispaa ya Ubungo imewaomba TARURA na TANROADS kuzibua mitaro ya barabara katika eneo la Ubungo Riverside ili kutatua changamoto ya kujaa mchanga kwenye mitaro hali ninayosababisha maji kutuama na kupelekea uwepo wa harufu mbaya inayokera wananchi
Aidha, katika kuhakikisha Ubungo inakuwa safi, Manispaa ya Ubungo inaendesha kampeni ya kataa uchafu, safisha pendezesha Ubungo (KAUSAPEU) inayolenga kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha maeneo yao ikiwemo maeneo ya biashara ili kuwa na mji safi lakini pia kuzuia magonjwa yanayosababishwa na uchafu.
Ufafanuzi huu umetolewa na Joina Nzali Mkuu wa kitengo cha mwasiliano serikalini- Manispaa ya Ubungo"
Kabla ya Usafi na uzibuani Mitaro
Baada ya Usafi kufanyika na uzibuaji Mitaro