Manispaa ya Ubungo yathibitisha ujio wa mvua kubwa za El Nino kuanzia Oktoba hadi Desemba, watoa tahadhari

Manispaa ya Ubungo yathibitisha ujio wa mvua kubwa za El Nino kuanzia Oktoba hadi Desemba, watoa tahadhari

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Manispaa ya Ubungo imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoweza kuambatana na hali ya El Nino katika msimu wa mvua unaotarajiwa wa Oktoba - Desemba, 2026

Tahadhari hiyo inafuatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa hali ya hewa na uwezekano wa kuwepo kwa mvua nyingi katika baadhi ya maeneo nchini.

Katika mazingira ya Manispaa ya Ubungo, mvua kubwa zinaweza kusababisha changamoto mbalimbali ikiwemo mafuriko katika maeneo ya mabondeni, kuziba kwa mitaro ya maji, uharibifu wa miundombinu, usumbufu katika usafiri pamoja na athari kwa makazi na shughuli za kiuchumi za wananchi.

Manispaa imewasisitiza wananchi kuhakikisha maeneo yao ya makazi na biashara yanakuwa katika hali salama kwa kusafisha mitaro na njia za maji, kuepuka kutupa taka katika mifereji ya maji na kutoa taarifa mapema endapo wataona maeneo yanayoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

Aidha, wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na maeneo mengine yanayoweza kuathiriwa na mafuriko wanashauriwa kuchukua tahadhari mapema na kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA pamoja na maelekezo kutoka kwa mamlaka husika.

Manispaa ya Ubungo pia inawahimiza wadau wa sekta mbalimbali, hususan usafiri, biashara, afya, elimu na ujenzi, kuzingatia utabiri wa hali ya hewa katika mipango yao ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa.

Manispaa ya Ubungo itaendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kutoa elimu na maelekezo kwa wananchi kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa salama na shughuli za kila siku zinaendelea kwa utulivu wakati wa msimu wa mvua.

ubungomanispaa_1788150395_3975616075980294734_42394184002.webp
 
Back
Top Bottom