timu zote viongozi longolongo tu. Kweli simba inakosa pesa za kulipia uwanja!? Ingawa nawapongeza wanachama kwa kupitisha mchango kwenye mkutano mkuu, tofauti na wenzao ambao wanataka walipiwe hadi mchango wa kadi za uwanachama ndo waende mkutanoni! Hivi pesa za samata, ochan, mrwanda na henry joseph ambazo zingetosha hata kwa uwanja wa mazoezi zimeenda wapi?na fedha za rambirambi je? Na yanga nao wanafukuza kocha bila kutathmini hasara watakayopata! Haya milioni 200 hizooo mtakatifu wenu tomasi anaondoka nazo! Klabu inamradi gani wakupata pesa zote izo?(kuna taarifa kuwa wamekopa, tayari deni ilo!), huku papic naye huyooo kakinukisha! Bila kusahau Njoroge yuko kwenye foleni anasubiri kukinga chake! Alaf ujengwe uwanja! What a hell is this!? Klabu imekua kama muembe wa uwani kila mtu anajitingishia tu! Eti kisa yeye ni Baniani! Mbona kuna kipindi aliitelekeza timu ikawa ina haha hadi wachezaji wakatoroka hotelini Arusha sababu ya deni! Huyo ameingia klabuni kufidia hasara alizopata kipindi kileee...amkeniiii! Baada ya mechi na JKT kuna watu wa yanga waKaanza kumuimbia na wengine kutaka hadi kumbusu...!! Bahati nzur aliwahi kupanda gari( alafu kuna jamaa anasema eti yanga hakuna watindiga! Hawa tuwaiteje? Mapoyoyooo au michelee!!?) maskini ya Mungu bado wamelala!