Manji ameipa klabu ya Yanga SC hekari 715 Geza Ulole

Manji ameipa klabu ya Yanga SC hekari 715 Geza Ulole

Naona yanga yaelekea kuwa chama cha wakulima maana kwaajili ya uwanja wa mpira heka 10 ni zaidi ya tosha
 
nimesoma mahali alikuwepo mke wa karume na mwigulu nchemba ndio walifungua hizo ekari wala sikuona habari ya manji kuwapeleka geza ulole....yaani ndala
 
Wakimataifaaaa...
Huko kutajengwa kila kitu kinachohusiana na michezo. Hao ndo umoja wa mataifa, GEZA ULOLE...
 
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Bw. Yusuph Manji ameikabidhi Yanga eneo la ekari 715 lililopo maeneo ya Gezaulole, Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo pamoja na kituo maalum cha kukuza vipaji vya michezo.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo kwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo mama Fatma Karume katika hafla fupi ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
IMG-20160928-WA0039.jpg
IMG-20160928-WA0041.jpg
IMG-20160928-WA0042.jpg
IMG-20160928-WA0044.jpg
IMG-20160928-WA0045.jpg


taarifa kutoka chanzo kimoja klabuni hapo imesema kuwa uzinduzi huo ulikuwa ufanyike 28 october kama ilivyoonekana kwenye jiwe la msingi ila mambo yamefanikiwa kufanyika upesi hivyo hakukuwa na haja ya kusubiri mpaka tarehe hiyo ifike
 
Timu ya Soka ya Yanga waanza rasmi ujenzi wa Uwanja wa Kisasa Kigamboni utakaokua na Hadhi ya Kimataifa. Akizungumza jana Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, alimshukukuru Mwenyekiti Manji kwa jitihada na pia Kuishukuru Kampuni ya International Village kwa kutoa Uwanja huo.

Hafla hiyo fupi ya uzinduzi ilihudhuria na Mama Fatma Karume pamoja na wanakamati wengine wa Bodi ya Wadhamini na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Hafla hiyo ambayo iliambatana na uwekaji wa jiwe la msingi ilikua ni ya kimya kimya na Yanga hata hawakualika Vyombo vya Habari. Taratibu zitaanza rasmi tarehe 28 Octoba, 2016.
 
Soon anga za Zamalek. TP Mazembe... Mechi na simba tunawapa tickets buku tu na za kimataifa tunajaza uwanja wenyewe bila ya Jezi ya Yanga sio ruksa
 
Ma
Hahaha! Jangwani city basi tena!anyway kama ni kweli sasa tunaanza kuona hatua za dhati na dhabiti kuikwamua Yanga,Lakini Ile habari ya jangwani city ilikuwa changa la macho ..!mabasi ya mwendo kasi yakae wapi?
Mwenyekiti Manji alitenga bilioni 52 kuwahamisha wakazi wa mtaa wa Twiga sio kule bondeni serikali ikanuna maana bila ya Yanga uwanja wao wa Taifa ungekuwa makumbusho... Sasa tunaenda kigamboni 2018 tutacheza mechi moja tu Taifa na simba ya ugenini
 
Afadhali Club zote zingejitambua kwa kujenga viwanja vyao ingekuwa byee sana hata ratiba zisinge badilishwa mara Kwa mara tungewaachia wenye viwanja waendelee na mabonaza yao!
 
Back
Top Bottom