Manji arejea Dar akiwa fiti
Habari Zinazoshabihiana
Nipo fiti, narejea leo-Manji 31.10.2008 [Soma]
Hali ya Manji bado tete 30.10.2008 [Soma]
Manji augua ghafla Dar 29.10.2008 [Soma]
Na Mwandishi Wetu
MFADHILI mkuu wa Klabu Bingwa ya Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam, Yusufu Manji, amerejea nchini kutoka Nairobi alikokuwa akitibiwa malaria katika hospitali ya Aga Khan.
Ndugu wa karibu wa mfadhili huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema Manji aliewasili Dar res Salaam juzi usiku kwandege, baada ya hali yake kuridhisha.
"Aliwasili juzi usiku wa saa tatu akitokea Nairobi na kwa kweli hali yake hajambo anapumzika kidogo na ataendelea na shughuli zake kama kawaida," alisema ndugu huyo.
Manji ambaye alikimbizwa Nairobi Jumatano iliyopita baada ya hali yake kubadilika ghafla na kukimbizwa Aga Khan Dar es Salaam, alikuwa akikiabiliwa na malaria kali.
Alipatwa na maradhi hayo siku moja tu baada ya timu ya soka ya Yanga kumlaza hasimu wake Simba kwa bao 1-0 katika uwanja mkuu wa Taifa Jumapili iliyopita.
Baada ya kubanwa na malaria, alikimbizwa katika hospitali ya Aga Khan ambako alilazwa siku moja na kupata nafuu akatolewa na kurudi nyumbani, lakini hali ilibadilika na kukimbizwa Nairobi.
Hata hivyo katika kile ambacho sasa kinaonekana kuwa ni mazoea kimaisha, baadhi ya watu walivumisha kuwa mfadhili huyo amefariki dunia.
Manji aliposikia habari hizo alisikitika na kuzikanusha huku akisema yuko fiti na alitarajia kurejea nchini juzi, kauli ambayo aliitekeleza.