Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimeangalia comments za ukurasa mmojawapo wa mitando ya kijamii kuhusu Manji kuzikwa Florida Marekani nimeshangaa kuona kundi kubwa sana la raia Watanzania hawana elimu kabisa kuhusu vigezo vya kuwa raia wa nchi hii au kuna ubaguzi mkubwa sana kwa raia walio wengi.
Wengi katika ukurasa huo wameshangazwa sana na kuuliza maswali kwamba kumbe Manji hakuwa Mtanzania?! Yani tuna raia wengi wanaojua kwamba Mtanzania hawezi kuzikwa nje ya Tanzania akifariki! Kwamba kigezo kimojawapo cha kuthibitisha Utanzania wako ni kuzikiwa katika ardhi ya Tanzania!
Sasa kama mtu amefikia kumiliki smartphone na hajui hata vigezo vya uraia wa nchi yake hao wengine watakuwa anafahamu nini katika masuala ya haki za uraia na mambo mazito ya katiba kwa ujumla?!
Itoshe kusema tuna safari ndefu kama nchi kuhusu katiba na elimu ya uraia.