maranguvillage
JF-Expert Member
- Sep 8, 2023
- 935
- 2,096
Life is a short trip
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uzi ufunguwe majibu yameshapatikana,,Ntaeleza kwa ufupi sana.
Yusuf Manji alikuwa na uraia wa Marekani na pia alibeba pasi ya kusafiria ya TZ. Hii ipo na sina haja ya kuilezea sana maana wengi wafanya hii kitu.
Hata Tundu Lissu nae ana pasi mbili ya Ubelgiji na ya Tanzania na abeba zote akisafiri.
Pili, baba yake Yusuf Manji Yusufali alikuwa ni raia wa Marekani ambako alienda kitambo sana na ana mali zake na familia yao karibu yote ipo huko na wali-settle sehemu ya Orlando Florida.
Huyo mtoto wake Mehbub nae huenda ana pasi mbili yaani ile ya Green Card na ya TZ ni kawaida kwani Green Card ni kwa permanent residency uraia wa kudumu.
Ukiwa ughaibuni na una uwezo waweza kununua eneo (kipande) kwenye makaburi ili siku ikifika wazikwa hukohuko juu kwa juu. Yusuf Manji amezikwa kwenye makaburi ya familia ya Manji karibu na alipolala baba yake Yusufali.
Huyo Mehbub nae Mungu akimchukua, ana kaburi lake tayari.
Kwahiyo suala hili si gumu kulielewa, ukiwa nje ya nchi na una makazi ya kudumu waweza kuamua kuzikwa hukohuko ili familia yako iwe na urahisi wa kufagia kaburi.
Zitaoelekwaje ubalozi wa Tanzania wakati ana passport ya marekani?kwahiyo wewe unatwambia kuwa Taarifa hazijapelekwa huko Unoalozi? umepata wapi hizo habari mkuu
Kwanza Dola ya Iran ni Dola ya Kishia. Pili, hakuna mtu au watu wanaoumiliki Uislam kama kabila. Kwamba wao tu ndio Waislam kwa hali yoyote. Uislam sio kabila ni Dini. Ina misingi yake na nguzo zake na taratibu zake. Yoyote yule anaweza kuwa Muislam bora bila kujali anatoka wapi au ni jamii gani. Cha msingi ni Uislam kama alivyokuja nao Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na wakaufuata Maswahaba zake (Allah Awaridhie).Iran islamic state,kule ndio uislamuni kwenyewe,huku kwetu uislam uliletwa na nashua
Salute kwako,uko deep mkuu ila hoja yangu ni kuwa nani yuko sahihi kwenye swala la mazishi,muislam wa Tanzania anayezikwa chapchap au wa iran anayezikwa baada ya siku tatuKwanza Dola ya Iran ni Dola ya Kishia. Pili, hakuna mtu au watu wanaoumiliki Uislam kama kabila. Kwamba wao tu ndio Waislam kwa hali yoyote. Uislam sio kabila ni Dini. Ina misingi yake na nguzo zake na taratibu zake. Yoyote yule anaweza kuwa Muislam bora bila kujali anatoka wapi au ni jamii gani. Cha msingi ni Uislam kama alivyokuja nao Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na wakaufuata Maswahaba zake (Allah Awaridhie).
Nasabu peke yake haimfai chochote mtu. Ndio maana Abu Lahab ataingia motoni licha ya kuwa ni baba yake mdogo Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), ila Bilal (Allah amridhie) mtu mweusi kutoka Afrika alikuwa Swahaba wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na atakwenda peponi.
Wala miji haitakasi watu ndio maana akina Abu Jahal watakwenda motoni licha ya kuwa waliishi Makkah na wakiishi jirani na Kaaba. Lakini walikuwa makafiri washirikina.
Allah amewanyanyua watu na kuwapa utukufu kwa huu Uislam, sio kwa sababu ya rangi zao wala makabila yao. Ndio maana waliposimama sawa na kuinusuru Dini yake akawanyanyua na kuwapa utukufu katika ardhi bila ya kujali rangi na makabila yao. Ndio maana walinyanyuliwa waturuki (Ottoman Empire, Saljuqs nk) kwa huu Uislam, walinyanyuliwa wahindi (Mughal Empire na wengineo) kwa huu Uislam, wakanyanyuliwa watu weupe akina Mamluks kwa huu Uislam, walinyanyuliwa wakurdi (akina Salahuddin) kwa huu Uislam, walinyanyuliwa watu weusi wa Afrika (akina Mali Empire na Songhai Empire na akina Uthman Dan Fodio nk), walinyanyuliwa Berbers akina Tariq ibn Ziyad walioifungua Spain, wakanyanyuliwa Al Murabituun (Al Moravid Dynasty) na kisha al-Muwahhiduun (AlMohad Caliphate) wote ni wa Berbers wa North Africa.
Bila kusahau wanachuoni kutoka jamii tofauti tofauti walioipigania Dini hii katika kila zama tokea mwanzo huko mpaka leo na kuacha mchango mkubwa.
Utukufu unatoka kwa Allah. Na wale waliopewa utukufu katika Dini hawakupewa utukufu kwa sababu ya makabila yao bali kwa sababu ya Dini hii.
Tunamshukuru Allah kwa neema ya Uislam. Na tunamuomba atufishe katika Uislam. Tunamuomba atufishe katika Tawheed na Sunnah. Aameen.
Mafundisho ya Uislam ni kuharakisha kumzika maiti.Salute kwako,uko deep mkuu ila hoja yangu ni kuwa nani yuko sahihi kwenye swala la mazishi,muislam wa Tanzania anayezikwa chapchap au wa iran anayezikwa baada ya siku tatu
Kuharakisha ndio masaa mangapi tangu afarikiMafundisho ya Uislam ni kuharakisha kumzika maiti.
As soon as possible. Akifariki tu watu waanze kumuandaa akazikwe.Kuharakisha ndio masaa mangapi tangu afariki
Zitaoelekwaje ubalozi wa Tanzania wakati ana passport ya marekani?
Manji amezikwa kama raia wa marekani na sio Mtanzania..
Kuna mtu alikuwa BOT aliitwa BALALI naye alizikwa huko huko...Inawezekana hawa Watanzania wana Jambo ila wameshindwa kuliweka vizuri ili liweze kueleweka.
Kufa, Kuzikwa Marekani, kuzaliwa na kukulia Marekani sio shida.
Shida inaanzia pale wanapojifanya Watanzania kama mimi na wewe lakini uhalisia uliopo ni Utanzania wa maslahi lakini mioyo yao haipo hapa nakupaona kama kwao.