Manji kuzikwa Marekani kumedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga. Tuna safari ndefu kama nchi katika katiba na elimu ya uraia

Uzi ufunguwe majibu yameshapatikana,,

Manji hakuwa Mtanzania
 
kwahiyo wewe unatwambia kuwa Taarifa hazijapelekwa huko Unoalozi? umepata wapi hizo habari mkuu
Zitaoelekwaje ubalozi wa Tanzania wakati ana passport ya marekani?

Manji amezikwa kama raia wa marekani na sio Mtanzania..
 
Iran islamic state,kule ndio uislamuni kwenyewe,huku kwetu uislam uliletwa na nashua
Kwanza Dola ya Iran ni Dola ya Kishia. Pili, hakuna mtu au watu wanaoumiliki Uislam kama kabila. Kwamba wao tu ndio Waislam kwa hali yoyote. Uislam sio kabila ni Dini. Ina misingi yake na nguzo zake na taratibu zake. Yoyote yule anaweza kuwa Muislam bora bila kujali anatoka wapi au ni jamii gani. Cha msingi ni Uislam kama alivyokuja nao Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na wakaufuata Maswahaba zake (Allah Awaridhie).

Nasabu peke yake haimfai chochote mtu. Ndio maana Abu Lahab ataingia motoni licha ya kuwa ni baba yake mdogo Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), ila Bilal (Allah amridhie) mtu mweusi kutoka Afrika alikuwa Swahaba wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na atakwenda peponi.

Wala miji haitakasi watu ndio maana akina Abu Jahal watakwenda motoni licha ya kuwa waliishi Makkah na wakiishi jirani na Kaaba. Lakini walikuwa makafiri washirikina.

Allah amewanyanyua watu na kuwapa utukufu kwa huu Uislam, sio kwa sababu ya rangi zao wala makabila yao. Ndio maana waliposimama sawa na kuinusuru Dini yake akawanyanyua na kuwapa utukufu katika ardhi bila ya kujali rangi na makabila yao. Ndio maana walinyanyuliwa waturuki (Ottoman Empire, Saljuqs nk) kwa huu Uislam, walinyanyuliwa wahindi (Mughal Empire na wengineo) kwa huu Uislam, wakanyanyuliwa watu weupe akina Mamluks kwa huu Uislam, walinyanyuliwa wakurdi (akina Salahuddin) kwa huu Uislam, walinyanyuliwa watu weusi wa Afrika (akina Mali Empire na Songhai Empire na akina Uthman Dan Fodio nk), walinyanyuliwa Berbers akina Tariq ibn Ziyad walioifungua Spain, wakanyanyuliwa Al Murabituun (Al Moravid Dynasty) na kisha al-Muwahhiduun (AlMohad Caliphate) wote ni wa Berbers wa North Africa.

Bila kusahau wanachuoni kutoka jamii tofauti tofauti walioipigania Dini hii katika kila zama tokea mwanzo huko mpaka leo na kuacha mchango mkubwa.

Utukufu unatoka kwa Allah. Na wale waliopewa utukufu katika Dini hawakupewa utukufu kwa sababu ya makabila yao bali kwa sababu ya Dini hii.

Tunamshukuru Allah kwa neema ya Uislam. Na tunamuomba atufishe katika Uislam. Tunamuomba atufishe katika Tawheed na Sunnah. Aameen.
 
Salute kwako,uko deep mkuu ila hoja yangu ni kuwa nani yuko sahihi kwenye swala la mazishi,muislam wa Tanzania anayezikwa chapchap au wa iran anayezikwa baada ya siku tatu
 
Salute kwako,uko deep mkuu ila hoja yangu ni kuwa nani yuko sahihi kwenye swala la mazishi,muislam wa Tanzania anayezikwa chapchap au wa iran anayezikwa baada ya siku tatu
Mafundisho ya Uislam ni kuharakisha kumzika maiti.
 
Kuna mtu alikuwa BOT aliitwa BALALI naye alizikwa huko huko...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…